November 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Majaliwa akagua ujenzi barabara ya njiapanda Iyula-Ileje

Na Mwandishi Wetu,Timesmajiraonline, Songwe.

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa leo Novemba 24, 2023 amekagua maendeleo ya ujenzi wa barabara inayounganisha maeneo ya Ruanda, Nyimbili, Hasamba, Izyila, Itumba yenye urefu wa kilomita 79.67.

Barabara hiyo ambayo pia itaunganisha maeneo ya Mahenje, Hasamba, vwawa kwa urefu wa Kilomita 31.9 inayojengwa kwa kiwango cha lami.

Akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Mbozi, Mkoani Songwe wakati wa ukaguzi huo, Waziri Mkuu Majaliwa amesema Jukumu lao wao kama wasaidizi akiwemo yeye na Mawaziri wakuu wa mikoa na Wilaya ni kuhakikisha miradi inakamilika na inaanza kazi.

“Toka Dkt. Samia alipoingia madarakani mwaka 2021 mpaka leo kwa fedha ambazo zimetoka, tunachotarajia ni kuona miradi ambayo imekamilika inaanza kutoa huduma”

Waziri Mkuu Majaliwa amesema Barabara hizo zinazojengwa ziko kwenye madaraja mbalimbali, ikiwemo barabara zinazounganisha vijiji na vijiji, Kata na Kata, pia Wilaya na wilaya, ambapo zinahudumiwa na TARURA .

“Wananchi miradi hii Rais Samia ameamua itekelezwe kwenye maeneo yenu na hasa Ile ambayo nyie kilasiku huwa mnaitumia ndiyo ambayo sasa tunaipa nguvu zaidi ili Kurahisisha mwenendo wa maisha ya kilasiku”

“Niwahakikishie wananchi kwamba Rais Samia Suluhu Hassan anania njema na anatamani watanzania muendelee kuishi katika maisha marahisi zaidi na anafanya maboresho katika maeneo haya ikiwemo barabara” Amesema Waziri Mkuu.

Awali Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Dkt. francis Michael, aliwapongeza watendaji wa Wakala wa Barabara nchini (Tanroad) Mkoa wa Songwe chini ya Kaimu Meneja wa Mkoa Mhandisi Suleiman Bishanga kwa utendaji mzuri.