December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Maimartha wa Jesse amfunda Kajala kuhusu Paula

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online

MTANGAZAJI mkongwe na msanii wa Bongo movie Maimartha wa Jesse, amemtaka msanii wa filamu hapa nchini Kajala Masanja kuacha kumshirikisha mtoto wake ajulikanaye kama Paula pindi anapofanya mambo yake binafsi.

Akimpa ujumbe huo kupitia kwenye Ukurasa wake wa Instagram Maimartha amesema, Kajala amekuwa na tabia ya kushirikiana na mtoto wake kila analolifanya hasa katika mambo ya kidunia ukizingatia mtoto wake bado mdogo na anahitaji mambo mengi ya kufunzwa ikiwemo Elimu.

“Kajala, Leo naomba niongee maongezi ya ushindi na wewe!!. Pole Sana wewe na mtoto leo (jana) mmeamkia Lupango. Hii inamaana kubwa Sana na sio nzuri kabisa kwa mtoto, Ni sababu kila ufanyalo unashirikiana na mtoto (Paula).

“Ngoja niongee kwa Upendo. Mtenge Paula kwenye Mambo yako ‘My dear’. Juzi kati tu nilikuona ukiwa visiwani Zanzibar (wewe, Konde, Paula na marafiki zake) kulikuwa na ulazima gani wa kuongozana na mtoto kwenye mambo yako?. Mtulize mtoto Nyumbani na mtengenezee mazingira ya utoto/ kwa Sasa ningetarajia umfurahishe mtoto wako kwa kupata Elimu Bora. Angepaswa kuzungukwa na walimu (Kama unavyosema anatarajia kuingia kidato cha tano.

“Sikupangii maisha ila najaribu kusema kama nilivyokemea kwa binti yako kutumiwa/kupigiwa video call za utupu na mpenzi wako. Binafsi naona Mungu bado anakupenda cha upole(Kajala). Amekupa nafasi ya pili usimlaumu mtu, wewe badilisha mfumo wa maisha unayoishi na mtoto, kuna mahali utamuepusha. Kumchunga mtoto sio lazima uongozane nae kila mahali.

“Kajala ulikuja vizuri sana naomba uendelee vizuri, Sababu una uwezo Mzuri Sana wa kufanya Mambo mazuri. Kilichokuletea Shida nahisi ni hasira za kuona jinsi mtoto wako alivyotumika. Kajala usijali amka, futa vumbi songa mbele. ‘Be more Smart’,” ameandika Maimartha.