Na Esther Macha, Timesmajira, Online, Mbeya
ZAIDI ya wanawake 3000 wanapata changamoto ya kuugua ugonjwa wafistula kila mwaka nchini na kati yao ni wanawake 1500 pekee ndiowanaopata matibabu ya ugonjwa huo na wengine kushindwa kutibiwakutokana na changamoto mbalimbali ikiwemo hali ngumu ya kiuchumi.
Hayo yalisemwa jana na Mwakilishi wa Chama cha Madaktari Bingwa waUpasuaji wa Fistula Tanzania, Dkt. Peter Majinge wakati wa uzinduzi wakambi ya wiki mbili ya kutoa huduma bure kwa wanawake wenye fistulamkoani Mbeya.
Kambi hiyo imewekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya,Kitengo cha Wazazi, Meta, ambako madaktari Bingwa wa upasuaji watakuwawakitoa huduma hiyo bure kwa kipindi cha wiki mbili mfululizo.
Kambi hiyo ya vipimo na matibabu inaungwa mkono na Mbunge wa vitimaalum mkoa wa Mbeya na Naib u Waziri wa Maji , Mhandisi marypriscaMahundi ambapo kampeni hiyo inakwenda na kauli mbiu ya ya fistulasasa basi .
“Kuna idadi kubwa ya wanawake ambao hawapati hudumayeyote ya matibabu ya fistula kutokana na changamoto za kiuchumi,umbali wa kwenda kupata huduma na ukosefu wa elimu ya upatikanaji wamatibabu ya ugonjwa wa fistula,” amesema Dkt. Majinge.
Dkt. Majinge amesema kuwa chama cha madaktari wa Fistula kupitiaufadhili wanaopata kutoka Shirika la Fistula Foundation la Marekani,wanaenda kwenye maeneo ambako kuna akina mamaambao wamekosa uwezo wa kwenda kupata matibabu ya fistula nakuwasaidia kuwatibu.
Hata hivyo amesema wadhahili hao hawalipi gharama zote za matibabu yafistula, hivyo kwa niaba ya chama hicho akaiomba serikali isaidiekusamehe baadhi ya gharama katikahospitali wanazokwenda kutoa huduma za matibabu ya fistula ili wawezekumudunia na kuwasaidia akina mama wengi zaidi.Pia ameomba taasisi za ndani ya nchi nazo ziungane na wadhadhili wanje kusaidia akina mama wenye tatizo la fistla kwa lengo la kutokomezaugonjwa huo nchini.
Naibu waziri wa maji Mhandisi, Maryprisca Mahundi ndiye aliyekuwamgeni rasmi kwenye uzinduzi wa kambi hiyo ambaye amesema kuwaataendelea kuwakwamua akina mama kimatibabu nakuimarisha afya za akina mama na kulinda uchumi wao.
Amesema ujio wa madktari hao moani Mbeya unakusudia kutoa matibabubure kwa akina mama zaidi ya 60, hivyo akawataka wanawake wenyechangamoto hiyo kujitokeza ili wapatiwe matibabu.
Hata hivyo Mhandisi Mahundi amesema ataendelea kupaza sauti katikamaeneo yote ya mkoa wa Mbeya na wilaya zake akiwaeleza akina mamakuwa huduma hiyo itakuwaEndelevu mkoani Mbeya.
Amesema hata baada ya kambi hiyo kumaliza muda wake mkoani Mbeya nakurejea Jijini Dar es Salaam, huduma hiyo itaendelea kutolewa katikahospitali ya wazazi Meta.
Mhandisi Mahundi amesema maendeleo makubwa yanayoendelea kwenye sektaya afya yameendelea kutokana na utendaji mkubwa Dkt. Rais Samia SuluhuHassan hivyo lazima tumpongeze Rais kwa kazi kubwa anayofanya.
Mganga Mkuu wa kitengo cha wazazi Meta ambayo ni sehemu ya hospitaliya Rufaa Kanda ya Mbeya, Dkt. Francis Rogoshora amesema kuwa Fistulani ugonjwa unaowapa mateso makubwa akina mama kwa sababu inasababishamaumivu makali kwa akina mama.
Dkt. Rogoshora amesema kitendo kilichofanywa na Naibu Waziri wa maji(Mb) Mhandisi Maryprisca Mahundi cha kushawishi madaktari hao bingwakupiga kambi mkoani Mbeya kwa lengo la kutoa matibabu ya fistula bure ni jambo kubwa la kuokoa wanawake wenye changamoyo hiyo.
More Stories
Kiswaga:Magu imepokea bilioni 143, utekelezaji miradi
Zaidi ya milioni 600 kupeleka umeme Kisiwa cha Ijinga
Kamishna Hifadhi ya Ngorongoro atakiwa kupanua wigo wa Utalii nchini