Na Esther Macha , Timesmajira Online, Mbeya
MBUNGE wa Vitimaalum Mkoa wa Mbeya ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maji Mhandisi, Maryprisca Mahundi amekipa tabasamu kikundi cha Vicoba cha wanawake Kata ya Iyela (KIWAKAI) kwa kuwaongezea mtaji wa milioni 1 na majiko ishirini na tano ya gesi ikiwa ni muendelezo wa kampeni ya kutunza mazingira na vyanzo vya maji.
Mhandisi Mahundi amesema kuwa amekuwa akijisikia fahari kuona wanawake wakipambana na kujishughulisha na kazi mbalimbali za kujiongezea kipato.
Mhandisi Mahundi amesema hayo leo wakati wa mkutano wa hadhara Kata ya Iyela jijini Mbeya ulioenda sambamba na kuzindua kikundi hicho cha vicoba.
Amesema kuwa nchi imezungukwa na wanawake majasiri na watafutaji ni jambo la faraja sana hivyo kama kiongozi Mwanamke lazima kuwaunga mkono kwa jitihada hizo.
Mbali na hayo amewapongeza wanawake kwa wazo la kujikwamua kiuchumi huku akijitolea kulipia kadi 100 za wanachama wa UWT waliomua kujiunga baada ya kufurahishwa na utendaji wa Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na kuwezesha vitenge zaidi ya 20 wazee.
Awali akisoma risala Leah Swillah amesema katika kikundi hicho wamefanikiwa kukusanya mtaji wa kiasi cha milioni 3,lengo likiwa ni kununua bajaji ili kukuza uchumi.
More Stories
Watoto wenye uhitaji wapatiwa vifaa vya shule
Wananchi Kisondela waishukuru serikali ujenzi shule ya ufundi ya Amali
RC.Makongoro ataka miradi itekelezwe kwa viwango