Na Joyce Kasiki,Timesmajira online
HAKIMU wa Mahakama ya Mtoto Orupa Mtae amesema,moja ya majukumu inayofanywa na mahakama hiyo ni kuangalia haki za mtoto hata kama ni mshtakiwa.
Akizungumza kwenye maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara kwenye banda la Mahakama jijini Dar Es Salaam ,Mtae amesema jambo la kwanza linaloangaliwa mara tu mtoto anapofikishwa mahakamani ni ustawi wake na kuhakikisha haki zake hazivunjwi.
“Sheria inataka mtoto anapokuwa Mahakamani awe na mzazi,mlezi au mwakilishi ambaye ni wakili wa utetezi na anapokuwa Mahakamani tunahakikisha anakuwa na mtu wa kusaidia katika mambo yote ya kisheria,” amesema Hakimu Mtae.
Amesema ,umuhimu wa mtoto kuwa na mzaz,mlezi mahakamani ni kumsaidia mtoto wakati ambao jambo lolote linaloweza kutokea.
Vile vile amesema,mtoto anapokuwa Mahakamani wanasikiliza kesi jinai ,mahakama hiyo wanahakikisha lugha inayotumika ni nyepesi na ya kueleweka kwa mtoto.
“Kwa ujumla yapo mambo mengi tunayoyaangalia kwa ajili ya kulinda haki za mtoto kama vile kuhakikisha mtoto haulizwi maswali yanayoweza kutweza utu wake, yakamfanya akaogopa ili kumuwekea mazingira ya kutoogopa hata kama amefanya kosa.” amesema na kuongeza
Aidha amesema katika mahakama hiyo huwekwa michezo mbalimbali ya watoto ikiwemo michezo kwani pia ni haki yake.
“Tunaposema mtoto ni yule wa kishuka chini ya miaka 18,kwa hiyo wapo watoto hadi wa chini ya miaka minne wanafikishwa mahakamani kwa changamoto mbalimbali,kwa hiyo hivi vitu ni muhimu sana kwa watoto ili wanapofika mahakama wasihisi kitu tofauti,lakini ni haki ya mtoto kucheza”.amesema
Pia amesema mahakama hiyo inasikiliza mashauri yote ya madai na jinai, ambapo mashauri ya jinai ni pale mtoto anapofanya kosa kinyume na Sheria ya kanuni ya adhabu .
More Stories
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba