Na Penina Malundo, TimesMajira Online
KUTOKANA na uwepo wa Muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar umeweza kuendelea kudumisha amani na mshikamano uliopo baina ya nchi mbili.
Kupitia Muungano huo umewezesha kupatikana kwa mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kuunganisha mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kuunganisha mataifa hayo mawili na kuunda Taifa moja lenye nguvu.
Mafanikio yaliyopatikana kutokana na muungano kati ya Tanzania Bara na Visiwani ni kukua kwa uchumi na kukabiliana na matatizo ya umasikini na ukosefu wa ajira,kuimarisha miundombinu ya usafiri wa anga,majini,kisiasa na nchi kavu.
Aidha Muungano umeimarisha na kuboresha upatikanaji wa huduma za jamii ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa idadi ya shule na hospitali pamoja na kukua kwa demokrasia nchini.
Katika mkutano wake wa kampeni uliofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja,Visiwani Zanzibar,mgombea Urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa nafasi ya Chama cha Mapinduzi,Dkt.John Magufuli kupitia Muungano Tanzania umeifanya kuwa taifa pekee barani Afrika ambalo mipaka yake haitokani na mipaka iliyowekwa na wakoloni.
Anasema muungano huo pia umewawezesha kudumisha uhusiano wa kindugu na kihistoria kati ya Wazanzibar na Watanganyika.
Dkt.Magufuli anasema endapo atachaguliwa atafanya kila liwezekanalo kuulinda,kuudumisha na kuundeleza muungano uliopo nchini.
Anasema atahakikisha analinda mapinduzi matukufu ya Zanzibar kwani Muungano kati ya Tanzania Bara na Visiwani umekuwa na faida kwa pande zote mbili.
Anasema Muungano huo umeifanya Tanzania kuwa taifa pekee barani Afrika ambalo mipaka yake haitokani na mipaka iliyowekwa na wakoloni.
Aidha anasema Muungano uliopo umewawezesha kudumisha uhusiano wa kindugu na kihistoria kati ya wazanzibar na watanganyika.
“Sababu iliyonileta huku nimekuja kumuombea kura mwanaCCM mwenzangu,mgombea wa urais Dkt.Hussein Mwinyi ili achaguliwe kuwa Rais wa Zanzibar ili nikashirikiane nae katika kuulinda muungano uliopo,”anasema na kuongoza;
“Pia ataweza kushughulikia changamoto zinazotukabili…mimi na Mwinyi tunafanana sababu sisi sote ni CCM,tutashirikiana vizuri kuimarisha muungano wetu na kuleta maendeleo ya kweli katika taifa,”anasema.
Aidha anasema Dkt.Mwinyi amekuwa waziri wa ulinzi miaka 11 akiwa chini ya wizara hiyo.
Anasema katika ilani yao itahakikisha kuwa Tanzania inaendelea kulinda uhuru wake,kudumisha Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar na kuimarisha Muungano uliopo wenye mfumo wa Serikali mbili.
Anasema CCM inaamini kwamba uzalendo kwa nchi msingi wa maendeleo ya kweli ya Tanzania ambayo yataletwa na Watanzania wenyewe .
“Nashangaa huku kuna baadhi ya watu wanasema hawezi…ameweza kumudu katika wizara hiyo ya ulinzi ashindwe kuongoza nchi…!Watani zangu watu wazuri huku ndio mnawapiga vita,Wazanzibar wanahitaji maendeleo na kama mnataka maendeleo ya kweli Unguja na Pemba chagueni Dkt.Mwinyi.
“Dkt.Mwinyi naomba nikuombe utakapofanikiwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar hakikisha makamu wako wa pili wa Rais anatoka Pemba,”anasema Dkt.Magufuli.
Anasema Unguja na Pemba mgawanyiko unatakiwa upotee kwani hili ni taifa moja ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa sababu kuna Tanganyika na kwa Zanzibar kuna Unguja na Pemba.
Anasema Dkt.Mwinyi ni chaguo sahihi ya kuongoza Zanzibar kwani ni kijana makini,mnyenyekevu,muadilifu,mchapakazi na asiependa uzembe.
Dkt.Magufuli anasema tangu muungano uanzishwe marais wote walioongoza Zanzibar wamekuwa ni wale waliozaliwa kabla ya muungano.
“Safari hii CCM,imeamua kumleta kijana aliyezaliwa baada ya Muungano ambaye ni Dkt.Mwinyi na hii inaendana na hali halisi ya Zanzibar ambapo takribani asilimia 70 ya Wanzanzibar wamezaliwa baada ya Muungano,”anasema na kuongeza
“Dkt.Mwinyi ni mtu sahihi anawakilisha kundi la waliowengi na anajua nini Wazanzibar wa sasa wanahitaji kuona maisha yao yakiwa yameboreshwa,huduma za kijamii ikiwemo afya,elimu na maji inapatikana kwa uhakika”anasema.
Ansema Dkt.Mwinyi anataka kuona Wazanzibar wanaondokana na umasikini na kuona fursa za kiuchumi na ajira zinaongezeka.
“Endapo mtamchangua Dkt.Mwinyi nitampa ushirikiano wa kutosha mkubwa sana katika kulinda na kutetea maslahi ya Zanzibar,” anasema
…..AKIZUNGUMZIA SUALA LA MAFUTA
Dkt.Magufuli anasema mafuta na gesi itakayopatikana Zanzibar yatakuwa ni ya Wazanzibar wenyewe.
Anasema wazanzibar wasidanganywe na kitu chochote na ndio maana mnahitaji mtu makini kama Dkt.Mwinyi ili rasilimari hii itakayopatikana iwe faida ya Wazanzibar.
“Sisi kule bara tuliliwa dhahabu kweli kweli,tulichezewa zikawa zinachimbwa na kupelekwa mpaka tulipokuja kubadilisha sheria ya madini na kuifanya madini na dhahabu kuwa mali ya Watanzania.
“Kwa suala hili la mafuta namuamini,hawezi kuja kubadilika sababu ya mafuta atayasimamia kwa maslahi ya Wazanzibar,”anasema.
Kwa upande wake mgombea Urais wa Zanzibar,Dkt.Hussein Mwinyi anasema katika kampeni zao wamekuwa wakinadi kwamba wataleta mapinduzi katika uchumi Wazanzibar.
“Nimekuwa nikisikia wenzetu wakiwa wanabeza maneno tunayoyasema na wanapotosha mambo mbalimbali kwamba hatuwezi kuleta uchumi wa blue.
“Wanasema hatuwezi kuleta mapinduzi ya kiuchumi hususani katika uchumi wa blue kwa sababu uvuvi kwenye bahari kuu ni suala la Muungano na kwamba hatutaruhusiwa kufanya yale amabyo tutataka kuyafanya,”anasema.
Anasema uvuvi katika bahari kuu ni suala la Muungano na limeumbiwa sheria na makao makuu yapo Zanzibar na katika hili hakuna shaka yoyote kwani mgao umepangwa vizuri,mamlaka itachukua asilimia 50,huku asilimia 50 iliyobaki itagwanyisha Zanzibar asilimia 20 na Bara asilimia 30.
“Meli zote zitakazofanya kazi hapa hazitakuwa na pingamizi lolote kuvua katika bahari kuu,”anasema.
Dkt.Mwinyi anasema pia wanazungumza juu ya gesi na mafuta,tayari sheria ya mafuta na gesi imeshapitishwa na Baraza la Wawakilishi na wataendeleza sekta hiyo ya mafuta na gesi kwa maslahi ya taifa hususani kwa Zanzibar.
Akizungumzia bandari anasema wanatarajia kujenga bandari kubwa visiwani Zanzibar.
“Lingine wapinzani wanalolipotosha katika Muungano,wanasema juu ya kujipanga kuondoa muundo wa Muungano kutoa Serikali mbili kwenda moja,jambo hili si kweli sera ya chama cha CCM ni muungano wa Serikali mbili,”anasema.
Dkt.Magufuli anasema amani na utulivu uliopo katika nchi ni zao la Muungano uliopo.
Anasema vyombo vya ulinzi na usalama ni Muungano,Jeshi limekuwa imara katika kulinda mipaka ya nchi,Polisi wamekuwa mahiri kuhakikisha usalama wa raia na mali zao.
“Muungano wetu umeleta umoja wa kitaifa kati ya Wazanzibar na watu wa bara katika kufanya shughuli mbalimbali hadi biashara,”anasema.
Anawahidi Wazanzibar endapo akichaguliwa katika Uchaguzi Mkuu atayaenzi mapinduzi yaliyopo na kuendeleza Muungano uliopo.
More Stories
Boost ilivyoboresha miundombinu ya elimu Ilemela
Samia apongeza walimu 5,000 kupatiwa mitungi ya gesi, majiko kutoka Oryx
Uwekezaji kwenye kilimo utatimiza ndoto ya Samia ya nchi kuwa ghala la chakula Afrika