Na Joyce Kasiki, TimesMajira,Online, Dodoma
RAIS John Magufuli anatarajiwa kulihutubia Bunge Ijumaa, hotuba ambayo inatarajia kuonesha dira ya Serikali yake katika kipindi uongozi wake wa pili cha miaka mitano katika Serikali ya Awamu ya Tano.

Kupitia hotiba hiyo Rais Magufuli anatarajia kuelezea utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Ratiba ya Rais Magufuli kuhutubia Bunge imetolewa leo na Spika wa Bunge, Job Ndugai wakati akizungumza bungeni kuhusu utaratibu utakavyokuwa kesho kutwa.
“Hotuba hii ni muhimu, lakini kupitia sisi wabunge anakuwa analihutubia Taifa, kwa hiyo naomba niwataarifuni kuwa kesho kutwa saa tatu kamili asubuhi tutawaomba waheshimiwa wote tuwe ndani ya ukumbi huu,” amesema Spika Ndugai.
More Stories
Dkt.Samia ahimiza wananchi kujitokeza kujiandikisha
Prof.Ndakidemi ashauri selimundu itibiwe bure
SGR yaiweka Tanzania Katika Ramani ya Usafirishaji wa Kisasa