November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Jonathan Shana

Magufuli chupuchupu awatumbue RPC, Kamanda TAKUKURU Arusha

Na Mwandishi Wetu

RAIS John Magufuli, amewataka Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Jonathan Shana na Kamanda wa TAKUKURU mkoani humo kubadilika na kufanyakazi walizotumwa kuzifanya na sio kufannyakazi wanaojituma wao.

Rais Magufuli, ametoa onyo hilo kwa viongozi hao leo, Ikulu jijini Dar es Salaa mara baada ya kumwapisha Mkuu mpya wa Mkoa wa Arusha, Idd Kamanta na kisha kushuhudia kuapishwa kwa viongozi wengine aliowateua.

Viongozo hao ni Mkuu wa Wilaya ya Monduli, DCP Edward Balele, Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Bakari Msulwa, Mkurugenzi wa Kaliua, Jerry Mwaga, Mkuu wa Mkoa wa Wilaya ya Arusha Mjiji, Kenan Kihongosi na na Mkurugenzi wa Jiji la Arusha, John Pima. ,

Rais Magufuli amesema, alikuwa awatoe kwenye nyadhifa zao viongozi hao, lakini amewasamehe, hivyo wanatakiwa kubadilika na kufanyakazi walizotumwa kuzifanya.

“Na kwa sababu mtu wa TAKUKURU yupo hapa (Brigedia Jenerali Julius Mbungo) na IGP (Simon Sirro) mkawaonye watendaji wenu wa Arusha, wafanyekazi walizopelekwa kufanya,” ameonya Rais Magufuli na kuongeza;

“Nilikuwa nimtoe Kamanda wa Polisi Arusha na Kamanda wa TAKUKURU, wafanye kazi nilizo watuma sio kazi wanazojituma wao. Haiwezekani watu uwatume kufanyakazi za Serikali wanaenda kufanya nyingine katika kipindi kifupi. Wafanye kazi kwa mujibu wa mamlaka yao, wasimamie maadili yao, nilikuwa niwatoe lakini nimewasamehe.”

Amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Kamanta kuwafikishia ujumbe viongozi hao ili wafanyekazi walizotumwa na sio zile ambazo wameanza kuzifanya siku za karibuni.