Na Doreen Aloyce, TimesMajira Online, Dodoma
Rais wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli amemuagiza Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Dkt. Harison Mwakyembe kuhamishwa kwa chombo kinachosimamia sanaa Tanzania (COSOTA) kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara kwenda Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Rais Magufuli amesema hayo leo Ikulu Chamwino katika ghafla ya chakula cha mchana alipokula na Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Halmashauri ya CCM kufuatia mualiko wake.
Amesema kuwa Waziri mwenye dhamana kabla ya kwenda kuchukua fomu ya kugombea Ubunge jimboni kwake anapaswa kupeleka barua ili aweze kuisaini.
“Niwapongeze wasanii mmeitangaza Tanzania kwa maslah mapana, Serikali iko pamoja nanyi kuhakikisha inatetema maslahi yenu, najua mmeteseka sana nahitaji mtoke huko COSOTA na kuingia kwenye Wizara ya Habari ili kazi zenu zionekene na mfaidike ” amesema Rais Magufuli.
Amesema COSOTA ilishindwa kuwasimamia vizuri wasanii na kazi zao jambo ambalo limesababisha wasanii kuteseka kwa muda mrefu kwani wapo waliotumia kazi zao kwa manufaa binafsi.
Amesema kuwa kuitoa huko itasaidia kwa kiasi kikubwa wasanii kuepukana na changamoto wanazokumbana nazo.
“Serikali inatambua kazi wanayofanya wasanii kwa kuitangaza Tanzania ndani na nje ya nchi hivyo niwatake kuendelea na ushirikiano wenu ili kulisongesha taifa mbele” alisema Rais Magufuli.Â
More Stories
Samia awazawadi Stars milioni 700/-
Samia atoa bilioni 8/- kukarabati viwanja vya CHAN, AFCON
Rasmi Chatsoko mdhamini mkuu wa Goba Hills Marathon 2025