Na Penina Malundo, TimesMajira Online, Dar es Ssalaam
TUME ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) imemtangaza Dkt. John Magufuli ameshinda kuwa Rais wa Tanzania kwa kushinda kura 12,516,252 huku akifuatiwa na Mgombea Urais kwa Tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Tundu Lissu akipata kura 1,933,271.
Mnamo Oktoba 28,2020 Watanzania waliungana kupiga kura kwaajili ya kuwachagua viongozi mbalimbali ikiwemo nafasi ya Urais, Wabunge, Wawakilishi na Madiwani kutoka sehemu mbalimbali ya nchi.
Akitangaza matokeo hayo leo jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa kimataifa wa Julius Nyerere,Mwenyekiti wa NEC , Jaji Mstaafu Semistocles Kaijage amesema baada ya kukamilisha zoezi la kuhesabu kura za uchaguzi mkuu huo,mawakala wamepewa matokeo hayo kutoka majimbo 264 nchi nzima na tayari kusaini matokeo hayo.
Wengine ni Leopard Mahona (NRA) 80,787, John Shibuda (ADA TADEA) 33,086, Muttamwega Mgaywa (SAU) 14,922, Cecilia Mwanga (Demokrasia Makini)14,556 , Yeremia Maganja (NCCR-Mageuzi) 19,966 , Ibrahim Lipumba (CUF) 72,885, Philipo Fumbo (DP) 8,283, Bernard Membe (ACT-Wazalendo) 81,129 na Queen Sendiga (ADC)7,627.
Wengine ni Twalib Kadege (UPDP) 6,194 , Hashim Rungwe (CHAUMMA) 32,878, Khalfan Mazrui (UMD) 3,721 na Seif Seif (AAFP) 4,635.
More Stories
Kiswaga:Magu imepokea bilioni 143, utekelezaji miradi
Zaidi ya milioni 600 kupeleka umeme Kisiwa cha Ijinga
Kamishna Hifadhi ya Ngorongoro atakiwa kupanua wigo wa Utalii nchini