Na Penina Malundo,TimesMajira,Online
MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt.John Magufuli, amesema kutokana na wasanii wa Mkoa wa Kigoma kukiunga chama chao mkono ni dhahiri watashida kwa kishindo katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu 2020.
Akizungumza katika uwanja wa lake Tanganyika jana,mkoani Kigoma,Dkt.Magufuli amewapongeza wasanii ambao wengi wao wanatokea Kigoma.
Amesema wasanii wanakiunga mkono Chama chao hivyo watapata ushindi wa kishindo katika uchaguzi huo.
“Wasanii hawa ni wa hapa wengi wamezaliwa hapa,tunaamini tunaenda kushinda nataka kuibadilisha zaidi Kigoma …tuchagueni sisi,”amesema Dkt.Magufuli.
“Nawapongeza wasanii wote wanaojitokeza kunadi sera za Chama cha Mapinduzi msiache kukipigia kura CCM,Oktoba28,mwaka huu,”amesema.
Wasanii waliopanda kunogesha jukwaa la mkutano wa Kampeni wa Chama hicho, Kundi la Wanaume kutoka TMK ,Linex Sunday ,Ali Saleh Kiba na Rajab Kahali(Harmonize).
More Stories
Kamati ya Mfuko wa Jimbo Musoma Vijijini yagawa vifaa vya ujenzi
Hatma mrithi wa Kinana kupatikana
Mrithi wa Kinana CCM kujulikana katika Mkutano Mkuu wa Jan 18/19