November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Magifti dabodabo chachu ya maendeleo nchini

WASHINDI wa kampeni ya Magifti Dabodabo wameeleza kuwa kampeni hiyo ya Tigo imeendelea kuwa chachu ya maendeleo katika kuwainua kiuchumi na kupata mitaji ya kuongeza na kukuza biashara zao.

Akizungumza leo Februari 02, 2024 mara baada ya kukabidhiwa milioni 5 Mkazi wa Mikocheni Jijini Dar es Salaam, Hemed Swai ameushukuru mtandao wa Tigo kwa kushinda kiasi hicho cha fedha jamba ambalo mara ya kwanza alipopigiwa simu hakuamini mpaka alipofika ofisi za Tigo.

Kampeni hiyo inayoendeshwa na Kampuni ya Tigo ilizinduliwa Mwishoni mwa Mwezi Novemba Mwaka jana huku ikimtambulisha Haji Manara kama SEMAJI la Kampeni hii, ambapo mteja wa Tigo anaweza kushinda Fedha Taslimu hadi Milioni 10, Safari ya Kwenda Dubai au Zanzibar, Set ya Vifaa vya Ndani ambavyo ni Sound bar, Friji, TV na Microwave na Zawadi kubwa ya Magari Mawili ( 0km ) ,

kingine kinachovutia katika kampeni hii ni kwamba ukishinda kitu kimoja wapo kati ya ivyo unamchagua na yeyote umpendae ili apewe zawadi iyoiyo uliyoshinda hii ndio maana halisi ya MAGIFTI DABO DABO.