*Ni ile aliyoagiza Rais Samia iundwe, ina wajumbe 19, kazi ya uoakoji ni usiku na mchana hadi mtu wa mwisho apatikane
Na Irene Clemence, Timesmajiraonline
WAZIRI Mkuu Kassium Majaliwa, ametangaza Tume watu, aliyoiunda kupitia maghorofa yote ya Kariakoo ambako biashara zinafanyika ili kujua ubora wa maghorofa hayo na shughuli zinazoendelea.
Majaliwa ametangaza Tume hiyo ikiwa ni utekelezaji wa maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan, aliyoyatoa akiwa nchini Brazil, alipokuwa kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano na Mjadiliano ya Mkutano wa G20.
Akizungumza kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam wakati wa kuaga miili 15 ya watu waliofariki kwenye tukio la kuporomoka kwa jengo la ghorofa Kariakoo, Majaliwa alisema Mwenyekiti wa Tume hiyo atakuwa Brigedia Jenerali Hoseah Ndagara, ambaye ni mkuu wa menejimeti ya maafa kutoka ofisi ya Waziri Mkuu
“Kwa maelekezo ya Rais Samia tumeunda Tume ya watu 19 ambayo watafanyakazi hiyo,” alisema Majaliwa.
Alisema Tume hiyo itasaidia Serikali kujua ni nini ifanye baada ya uchunguzi kwa sababu mahitaji ya soko la Kariakoo bado yako pale pale na ni soko la kimataifa kwa sasa linategemewa na nchi zote jirani zinazotunguka, kwa hiyo tunayo sababu ya kuliimarisha, kutambua ubora wa majengo ili wajasiriamali waendelee kufanyabiashara za kwa miongozo mipya na iliyotolewa baada ya Tume hiyo kutoa miongozo kwa Serikali.
***Mmiliki wa jengo
Aidha, Waziri Mkuu Majaliwa, alisema sambamba na hatua hiyo, Serikali inakamilisha taratibu za kufanya uchunguzi maalum wa chanzo cha ajali katika eneo hilo.
“Na katika hili nimeliagiza Jeshi la Polisi kumtafuta mwenye jengo popote alipo ili kulisaidia Jeshi la Polisi ili kujua ni kwa nini jengo limeanguka , watakuwa na maswali ya msingi na yeye atashiriki kujibu moja baada ya jingine,” alisema.
Akifafanua zaidi wakati akizungumza wakati wa kuaga miili hiyo Majaliwa, alisema amemwakilisha Rais Samia, kuaga miili ya watu 15 ambapo mmoja wa 16 umeishachukuliwa na ndugu.
More Stories
Kamishna Hifadhi ya Ngorongoro atakiwa kupanua wigo wa Utalii nchini
Wakuu wa Wilaya,Wakurugenzi watakiwa kusimamia programu za chakula shuleni
Mbowe akuna wengi kuhusu maridhiano