Na Yusuph Mussa,Timesmajiraonline,Kilindi
MADIWANI wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilindi mkoani Tanga wamebariki rasimu ya bajeti kwa mwaka wa fedha 2025/2026 ya sh. 36,855,233,537 kutoka kwenye vyanzo mbalimbali ikiwemo Serikali Kuu na Mapato ya Ndani ya Halmashauri.
Kiasi cha sh. 3,561,693,000 kinategemewa kukusanywa kutokana na vyanzo vya mapato ya ndani ya halmashauri ikiwemo sh. 2,922,270,928 kutoka katika vyanzo huru, na sh. 639,422,072 kupitia vyanzo lindwa.
Hayo yamesemwa Januari 29, 2025 na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilindi Idrissa Mgaza wakati anasoma bajeti hiyo mbele ya kikao cha bajeti cha Baraza la Madiwani, na kuongeza kuwa kiasi cha sh. 1,168,908,371 kinachotokana na mapato ya ndani sawa na asilimia 40, kimetengwa kwa ajili ya kuchangia shughuli za maendeleo.
“Katika mwaka wa fedha 2025/2026, Halmashauri ya Wilaya ya Kilindi imekasimia kukusanya jumla ya sh. 36,855,233,537 kutokana na vyanzo vifuatavyo. Kiasi cha sh. 3,561,693,000 kinategemewa kukusanywa kutokana na vyanzo vya mapato ya ndani ya halmashauri ikiwemo sh. 2,922,270,928 kutoka katika vyanzo huru, na sh. 639,422,072 kupitia vyanzo lindwa.
“Fedha za Ruzuku kutoka Serikali Kuu, miradi ya maendeleo sh. 8,481,935,202, matumizi mengineyo sh. 2,682,673,335, mishahara (PE Grants) sh. 22,082,132,000, na GPE- TSP sh. milioni 46.8, na kufanya jumla ya sh. 33,293,540,537,”amesema Mgaza.
Amesema, mchanganuo wa matumizi kwa miradi ya maendeleo. Miradi ya maendeleo, Mipango sh. milioni 20, miradi ya Kilimo na Mifugo sh. 182,181,278, miundombinu elimu msingi sh. milioni 250, miradi ya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu sh. 292,227,093, miradi ya afya sh. milioni 282, miundombinu elimu sekondari sh. milioni 112.5, na miradi ya maendeleo, Utawala sh. milioni 30.
Mgaza amesema kwenye bajeti ya 2024/2025, halmashauri hiyo ilikasimia kukusanya sh. 36,435,523,204 kutokana na vyanzo mbalimbali ikiwemo mapato ya ndani, mishahara, matumizi mengineyo pamoja na miradi ya maendeleo.
“Hadi kufikia mwezi Desemba, 2024, halmashauri imekwishapokea na kukusanya jumla ya sh. 18,451,034,220 sawa na asilimia 50.64 ya malengo. Kati ya fedha hizo, sh. 1,577,045,230 kinatokana na mapato ya ndani, sh. 11,211,842,358 ni mishahara, sh. 1,983,811896 ni matumizi mengineyo, na sh. 3,678,334,736 ni miradi ya maendeleo,”amesema Mgaza.
More Stories
Premium Active Tanzania yapunguza uhaba wa madawati Mlele
TARURA Kilindi kutumia bil.5.2 bajeti 2025/26
THBUB yatoa tamko kulaani mauaji ya Jumanne Juma