November 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Madiwani Halmashauri ya Jiji wakubaliana kumaliza migogoro ya mipaka

Na Heri Shaaban (Ilala ),Timesmajira

BARAZA la Madiwani wa Halmashauri Jiji Dar es Salaam limeazimia kumaliza migogoro ya Mipaka katika Halmashauri ambayo imekuwa Changamoto kubwa kwa eneo hilo.

Hayo yalisemwa na Mwenyekiti wa Kamati za Mipango Miji na Mazingira, Nyasika Getama, katika kikao cha Baraza la Madiwani Ukumbi wa Mikutano Arnatoglou Wilayani Ilala Leo wakati wa kuwasilisha Taarifa za Kamati katika baraza hilo.

Mwenyekiti Nyasika ameomba Baraza hilo kufanya utaratibu wa Kumaliza utatuzi wa kero hizo ambazo baadhi ya maeneo imekuwa changamoto.

“Maazimio ya Kamati ya Mipango miji na Mazingira kumaliza migogoro ya Mipaka na kuunda Kamati ndogo kumuona Mkuu wa Wilaya ya Ilala Arch,Ng’Wilabuzu Ludigija na Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam Amos Makala kwa ajili ya kutatua kero ya Mipaka ” amesema Nyasika .

Aidha Nyasika amesema pia Kufanya ziara ya kukagua hali ya Mazingira Viwandani kujenga Vikuko vyote kata za pembezoni ,wapewe mafunzo juu ya Master Plan ya Jiji .

Pia wamependekeza Ufukwe wa Bahari ya Hindi utengezwe uwe unafanana Bandari Salama sambamba na Shule na Vituo vya afya zijengwe kwa golofa .

Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Omary Kumbilamoto akizungumza na Naibu Meya wa Halmashauri ya Jiji Hilo (Kushoto)Ojambi Masaburi katika kikao Cha BARAZA la Madiwani ukumbi wa Arnatoglou Wilayani Ilala Leo Novemba 16/2022(NA HERI SHAABAN)

Mwenyekiti Nyasika pia amesema katika baraza hilo Wakuu wa Idara wapewe vifaa na usafiri kwa ajili ya utekekezaji wa Majukumu yao .

Diwani wa Kata ya Kivukoni Sharik Choughule ametoa kero ya Maji katika Jiji la Dar es Salaam akiomba Baraza la madiwani kuchukua hatua za haraka kutokana na Wananchi wa Jiji hilo kupata tabu ya Maji .

Diwani Sharik pia ametoa kero nyingine kuhusiana na Watoto wa mitaani ameshauri Baraza la madiwani watenge shule kwa ajili ya watoto hao.

Meya wa halmashauri ya Jiji la Dar es Salasm Omary akumbilamoto amesema kwa sasa visima vya maji vyote vipo chini ya DAWASA amempongeza Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan na Waziri wa Maji Abdalah Uwesu kwa mikakati waliochukua kuiwezesha Dar es Salaam iweze kupata maji kutoka Wilayani Kigamboni

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji Amani Mafuru amesema Rais Samia amezindua maji Kigamboni Bomba la Baharini baadhi ya Watu Upanga ,Samora na baadhi ya maeneo wameshapata maji Tabata wameanza kuweka Katika mtandao .

MWENYEKITI wa Kamati za Mipango Miji na Mazingira Nyasika Getama akiwasilisha Taarifa za Mipango Miji katika kikao cha Baraza la madiwani Halmadhauri ya Jiji Leo Novemba 16 Ukumbi wa Mikutano Arnatogulo (Na Heri Shaaban)

Amesema Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Amos Makala amefanya ziara ruvu katika kuangalia sehemu yanapozalishwa maji ambapo amekutana na Uharibifu mkubwa umefanyika Katika maeneo hayo na wafugaji.

Kaimu Mkurugenzi Mafuru pia amesema kuhusiana na Watoto wa mitaani Serikali na Wizara ya Maendeleo ya Jamii inafanya mpango kwa ajili ya kuwaweka sehemu sahihi.