Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online-Dar
Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Dar-es-Salaam wapitisha makadirio ya mpango wa bajeti ya shilingi bilioni 328.4 kwa mwaka wa fedha 2026 /2027,fedha hizo zimeelekezwa katika miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo sekta ya afya na sekta ya elimu.
Akizungumza katika kikao cha Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Jiji la Dar-es- Salaam,Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Elihuruma Maberya,amesema katika bajeti hiyo ya shilingi bilioni 328.4 mchanganuo wake sekta ya afya shilingi bilioni 16, miundombinu ya barabara bilioni 19 ,mikopo shilingi bilioni 11,idara ya elimu sekondari bilioni 16 na elimu msingi bilioni 16.

” Nawaomba Madiwani twendeni tukasimamie miradi ya maendeleo katika bajeti hii ya mwaka wa fedha 2026 /2027,ikatekeleze ilani ya Chama Cha Mapinduzi katika kata zetu 36,”amesema Maberya.
Pia amesema, Halmashauri hiyo imetenga bilioni 5,ikiwa ni utekekalezaji wa agizo la Rais alililitoa hivi karibuni wakati akifungua soko la Kimataifa la Kariakoo,ya kutaka iongezwe asilimia 5 kwa ajili ya kujenga masoko.
Diwani wa Kata ya Kipunguni Steven Mushi,amesema bajeti hiyo imegusa sekta zote ikiwemo elimu,miundombinu ya barabara ,masoko na mikopo ya asilimia ,10 ambayo inatolewa ngazi ya halmashauri.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo,amesema katika fedha hizo shilingi bilioni 4 zinaenda kujenga vituo vya afya vya kisasa na shilingi bilioni 11 zimeelekezwa katika mikopo ya asilimia kumi ambayo inatolewa ngazi ya halmashauri kwa wanawake,vijana na watu wenye ulemavu.

Mpogolo,amewataka Watendaji wa Ilala na Madiwani kwenda kusimamia bajeti hiyo ili iweze kutekeleza miradi ya maendeleo ya wananchi.
Mstahiki Meya wa Jiji la Dar-es-Salaam Nurudin Bilal(Sheta),amesema kila kata wananchi wanaenda kunufaika na bajeti hiyo kwani imegusa huduma za kijamii.


More Stories
TUCASA yaomba kuanzishwa sheria malipo sekta ya ujenzi
Kihongosi:Uhai wa chama mashina
Kihongosi: Msigombane kwa itikadi za vyama