November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Madaktari bingwa kutoka Ujerumani kuweka kambi ya upasuaji mtoto wa jicho Mbeya

Na Esther Macha, Timesmajira, Online, Mbeya

NAIBU wa Waziri wa Maji Mhandisi Maryprsca Mahundi (Mb) kupitia Taasisi yake ya Maryprisca women Empowerment Foundation (MWEF)kwa kushirikiana na hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya na madaktari bingwa kutoka nchini Ujerumani imeandaa kambi maalum ya uchunguzi na upasuaji wa mtoto wa jicho bure kwa wananchi.

Katikati ni Ofisa Mawasiliano na Uhusiano hospitali ya Rufaa Mkoa wa Mbeya ,Agrey Mwaijande akitoa taarifa kwa waandishi wa habari juu ya ujio wa madaktari bingwa kutoka Ujerumani

Akitoa taarifa leo kwa waandishi wa habari Ofisa Mawasiliano na Uhusiano wa hospitali ya Mkoa wa Mbeya , Agrey Mwaijande amesema kuwa kuanzia Agosti 22 mpaka 29 kutakuwa na madaktari bingwa wa macho kutoka nchini Ujerumani ambao wataweka kambi mkoani mbeya

‘’Kambi hii ya macho itaenda kufanya upasuaji wa mtoto wa jicho kwa wale ambao watagundulika na changamoto hiyo, inawezeshwa na Mbunge ambaye ni Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi kwa kushirikiana na uongozi wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya ambao kwa pamoja wakaona ipo haja kwa ya kusaidia wananchi kwani imeonekana kwamba kuna changamoto watu wengi kuogopa gharama za kupima macho na upasuaji wa mtoto wa jicho,’’amesema Mwaijande.

Amesema kuwa kupitia ushirikiano wa madaktari wenyeji na madaktari bingwa kutoka Ujerumani kutawekwa kambi katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa iliyopo eneo la Forest mpya kuanzia tarehe 22 Agosti mpaka 29.

Kushoto ni Mratibu wa Huduma ya Afya ya macho hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya,Dkt.Fariji Killewa

Mratibu wa Huduma ya afya ya macho Hospitali ya Rufaa ya mykoa wa Mbeya , Dkt. Fariji Killewa amesema kuwa katika kambi hiyo watakuwa na madaktari bingwa kutoka Ujerumani watatu na manesi wa kutosha kutoka hospitali ya mkoa na madaktari wenyeweji wawili .

Akizungumzia kuhusu tatizo la macho na mtoto wa jicho amesema kuwa ni kubwa ambapo mwaka 2022, kwa hospitali ya Mkoa walitibu wagonjwa 2,399 waliokutwa na mtoto wa jicho ni 622 na hao walifika hospitali wenyewe.

Pia waliofanyiwa upasuaji wa mtoto jicho kwa Mkoa mzima walikuwa 1,429 na kuwa waliweza kufanyiwa upasuaji wagonjwa wengi kutokana na kupata wadau wengi wa kuwasaidia Wilaya ya Mbarali ambako waliweka kambi mara mbili mwaka 2022 ambao walikuwa zaidi ya 600 na mara moja kwa mwaka ambao walikuwa 2023 417 .

Aidha amesema kuwa wagonjwa wengi wenye matatizo ya macho wanapata ugonjwa huo wakiwa na umri wa miaka 55 na kuendelea hivyo wazee wengi wanaachwa nyumbani na hawafiki hospitali hivyo kwasababu uchumi ni changamoto matibabu hayo ya macho yatafanyika bure.

Amesema kuwa ujio wa madaktari bingwa kutoka Ujerumani utaongeza ufahamu na uzoefu kutoka kwa wataalam wa kitaifa na utaongeza uwezo wa wafanyakazi wa ndani na kusaidia kugundua matatizo ya macho na kuyatatua kwa ufanisisi zaidi .

Diwani Viti Maalum Mbeya Jiji ,Fatuma Bora ambaye ni Mratibu ofisi ya Mbunge wa Vitimaalum Mkoa wa Mbeya akitoa ufafanuzi wa kambi hiyo ya macho

Vilevile amesema kuwa upatikanaji wa huduma za uchunguzi wa macho bila malipo utawezesha watu wengi ambao wamepata shida kutokana na gharama kubwa za matibabu ya macho kuweza kufanyiwa uchunguzi na kupata matibabu stahiki bila kujali hali zao kiuchumi.

Diwani wa Vitimaalum Mbeya ambaye ni Mratibu wa Ofisi ya Mbunge wa viti maalum ,Fatuma Bora amesema kuwa Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprsica alianza na program ya fistula ambayo iliwatibu wanawake wote wa Mkoa wa Mbeya wenye tatizo hilo.

Pia ameeleza kuwa watu wengi wanakuwa vipofu pasipo kutarajia baada ya kuona changamoto kubwa ya macho mkoa wa mbeya wanashindwa kumudu gharama za matibabu na kubaki kujifungia ndani hivyo ni ni vema wananchi wote wakajitokeza kutibiwa bure .

“Awali Mbunge wetu Mhandisi Mahundi alianzisha programu ya matibabu ya wanawake wenye fistula lakini kwasababu alikuwa na maono ya kuwasaidia wanawake lakini kapata wazo lingine kubwa ameleta programu nyingine ya uhusiano na kusema kuwa wagonjwa wengi wa macho wanakuwa vipofu kwa kuogopa gharama za matibabu,”.

Hii ni huduma ya pili kutolewa bure na taasisi ya Maryprisca Mahundi baada ya awali ya wagonjwa wa Fistula kutolewa bure kwa ushirikiano na Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya mapema mwaka huu katika hospitali ya wazazi Meta .