Na Jackline Martin, TimesMajira Online
UONGOZI wa Machinga Mkoa wa Dar es Salaam kupitia kamati zake mbalimbali za maandalizi umekanusha tamko lililotolewa Shirikisho la Umoja wa Wamachinga Tanzania ambalo limeleta taharuki kwenye tasnia ya machinga na mihimili ya wadau wakiwemo TANTRADE kuhusu kutokushiriki kwa Wamachinga katika Maonesho ya Kimataifa ya Biashara kwa mwaka huu .
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Wamachinga Mkoa wa Dar es Salaam Namoto Namoto alisema wao kama shirikisho la machinga Mkoa wa Dar es Salaam wana mahusino mazuri sana na TANTRADE hivyo taarifa iliyotolewa ilikua ikihatarisha mahusiano yao na TANTRADE lakini pia imeleta mkanganyiko hata mwa uongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam.
Namoto alisema uongozi wa Wamachinga mkoa upo tayari kushiriki katika maonyesho hayo yajayo na kubainisha kuwa taaarifa zilizosambaa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii si rasmi na hazikufuata utaratibu na kubainisha kuwa mpaka sasa TanTrade bado hawajabainisha kiwango cha ushiriki kwa Wamachinga kwa mwaka huu.
Kiongozi huyo wa Machinga Mkoa wa Dar es Salaam aliwataka viongozi wa Shirikisho la Wamachinga kufanya kazi kwa weledi na kufanya kazi Kwa kufuata misingi, taratibu pamoja ushirikishwaji katika upatikanaji wa taarifa sahihi.
Mbali na hayo,Namoto alisema wao kama shirikisho wapo katika mchakato wa kufanya maombi mbalimbali ya kuomba punguzo la ushiriki katika Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara ya mwaka huu 2022.
Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara katika Mkoa wa Dar eas Salaam hushirikisha wafanyabiashara mbalimbali wa ndani na nje ya nchi huku wamachinga wakitengewa eneo lao rasmi kufanyia biashara zao.
More Stories
CP.Wakulyamba ashuka Katavi na Nguzo nne za Uongozi
Zanzibar kuzalisha wachezaji wenye vipaji
Maandalizi ya mkutano mkuu CCM yapamba moto