Na Israel Mwaisaka, Timesmajira Online,Nkasi
KAIMU Mkuu wa Wilaya Nkasi ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kalambo mkoani Rukwa Razaro Komba amepiga marufuku kwa Mabaraza ya Ardhi ya Kata kutoa hukumu badala yake yajikite kwenye usuluhishi ili kuweza kuleta utengamano katika jamii.
Agizo hilo amelitoa Aprili 8,2024 wilayani Nkasi kwenye mkutano wa wadau wa kujadili mradi wa utekelezaji wa uboreshaji usalama wa milki za ardhi wilayani humo ambapo amesema kuwa lengo la serikali kuanzisha mabaraza hayo lilikua ni zuri kinyume chake yamekua chanzo cha kukuza migogoro.
Amesema kuwa mabaraza hayo yalipewa dhamana ya kusikiliza kesi na kutoa maamuzi lakini mwaka 2021 serikali ilibaini udhaifu na kuyaondolea nguvu ya kutoa maamuzi na badala yake yajikite kwenye usuluhishi pekee.
Kufuati hali hiyo ameiagiza Halmashauri ya Wilaya hiyo kupitia kitengo cha sheria kufikia Ijumaa ya wiki hii iwe imetoa mafuzo kwa Wenyeviti ,makatibu na wajumbe wote wa mabaraza ya kata ili kuwajengea uwezo wa kisheria namna ya kusuluhisha migogoro ya ardhi inayofikishwa katika mabaraza yao.
Pia amedai kuwa ardhi ina mchango mkubwa katika shughuli mbalimbali za maendeleo hivyo ni lazima ikatengenezewa utaratibu madhubuti wa kuilinda na kuwa mradi huo wa uboreshaji wa usalama wa miliki za ardhi ni suluhisho la tatizo hilo .
Pia ameeleza kuwa mradi huo ambao utadumu kwa muda wa miaka mitano ni lazima wahakikishe kuwa unaleta tija na miliki zitakazopatikana ziwasaidie wananchi katika kujiletea maendeleo katika nyanja mbalimbali kwani inagusa kila sekta.
Meneja Msaidizi wa mradi huo toka makao ardhi Patrick Mwakilili amedai kuwa wao watahakikisha mradi huo wa( LTIP) unawafikia wanananchi wote na kuona changamoto katika sekta hiyo ya ardhi inapungua kwa kiasi kikubwa hasa baada ya mpango wa matumizi sahihi ya ardhi utakapokamilika.
Meneja huduma kwa wateja wa NMB wilayani Nkasi Marijani James ameeleza kuwa mradi huo wa usalama wa miliki ardhi una fursa pia kwao kwa maana wataweza kutoa mikopo zaidi kwa wananchi ikiwemo mikopo ya kilimo na ufugaji yenye riba ndogo sana ukilinganisha na mikopo ya aina nyingine.
Amefafanua kuwa mikopo ya kilimo na mifugo utozwa riba ya asilimia 9 ukilinganisha na riba ya mikopo ya biashara riba ni asilimia 21 na mingine riba ni asilimia 23 na kuwa kwa mwaka 2023 wameweza kutoa mikopo ya Bil.4 kwa Wakulima na wafugaji wa wilaya Nkasi.
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi