June 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mabadiliko ya tabianchi,changamoto kubwa kwa watu wenye ulemavu

Na Penina Malundo, Timesmajira

TAASISI mbalimbali za masuala ya mazingira zinasema mabadiliko ya tabianchi yamekuwa yakiathiri moja kwa moja watu wenye ulemavu kwa nyanja ya Kijamii na Kiuchumi.

Hali hiyo ilimtokea Waziri wa Israel Karine Elharrar ambaye aligonga vichwa vya habari duniani kote baada ya kubainika kuwa hangeweza kuhudhuria mkutano wa kilele wa COP26 kwa sababu hakukuwa na miundombinu ya kumfanya ahudhurie kwa kutumia kiti chake cha magurudumu.

Kupitia mkutano huo ulionesha ni namna gani walemavu wengi,walihisi kupuuzwa au kuwekwa nje ya mazungumzo kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa ambayo yamekuwa yakiwaathiri wao kwa kiasi kikubwa.

Kwa mujibu wa Baraza la Haki za Kibinadamu la Umoja wa Mataifa,linasema walemavu ni miongoni mwa wale walioathirika zaidi katika hali ya dharura za mabadiliko ya hali ya hewa hivyo jitihada za ushirikishwaji juu ya majanga hayo wanapaswa kushirikishwa.

Kuna dharura mbalimbali zinaweza kuwakumba ikiwemo moto wa porini,mafuriko,mvua nyingi zinaweza kuwa za mara kwa mara,hali ya ukame hususan uwepo wa jua kali katika maeneo mengi.

Katika mkutano wa mabadiliko ya hali ya hewa wa COP26, baadhi ya maeneo yaliyogusiwa masuala ya watu ulemavu na mabadiliko ya hali ya hewa ambapo iliguswa katika suala la miundo jumuishi ya miji inayostahimili hali ya hewa na athari za mabadiliko hayo kwa afya ya watu wenye ulemavu.

Mara nyingi serikali hazifikirii kuhusu “mahitaji mahususi ya watu wenye ulemavu kipindi hiki cha dunia inavyokabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kuwaweka nyuma katika mipango mahsusi.

Miongoni mwa changamoto ni kukosekana kwa motisha na utashi wa kufanya mabadiliko katika ngazi ya mtu binafsi na kisiasa katika kuhakikisha watu wenye ulemavu nao wanapewa haki sawa kama wengine ya kujumuisha katika mabadiliko ya tabianchi.

Mwenyekiti wa Shirikisho la Watu wenye Ulemavu Taifa (SHIVYAWATA),Ernest Kimaya anasema mabadiliko ya Tabianchi yanaathiri watu hususan watu wenye ulemavu pale ambapo yanatokea na kufanya mabadiliko katika ardhi kuleta mchafuko ya mvua nyingi,jua kali na kusababisha ukame mkubwa ambapo watu wenye ulemavu kushindwa kuhimili matukio hayo mabaya.

Anasema kutokana na watu wenye ulemavu kuishi kwa mazoea,hali hiyo imekuwa inawaathiri kwa kiasi kikubwa na kuwafanya kuzidi kuwarudisha nyuma kiuchumi kutokana na kutumia gharama kubwa .

“Mabadiliko ni shida kwetu na hayataki tuishi kwa mazoea kwani kuna Changamoto kubwa watu wenye ulemavu,ukiangalia watu wenye ulemavu
hasa wanaotembea na fimbo nyeupe wanaweza kuleta shida,kutokana na utelezi na kama wakiweka fimbo wanaweza kupata shida,”anasema.

Pia anasema changamoto zinaenda kwa kutegemea jua likiwa kali watu wanapata athari kubwa ya uchumi kwani lazima wapate usafiri ambao utawasaidia katika shughuli zao hususani wale wanaoishi katika maeneo yenyewe mafuriko.

Anasema kundi hilo katika kushirikishwa kwenye Idara ya Menejimenti ya Maafa na serikali sio sana na hata wakishirikishwa katika utoaji wa maoni bado uwa hawaonekani katika kuteleza maagizo hayo kama na wao wasimamizi wa maamuzi ya maoni walioyatoa.

Anasema kuna umuhimu Idara hiyo kuwaigiza watu wenye ulemavu katika kuona namna na wao wanashirikishwa katika kupima maoni yao na kuona namna yanavyotekelezwa maafa yanapotokea.

Aidha Mwenyekiti huyo anasisitiza watu wenye ulemavu wanapaswa kujitahidi kuwa na tahadhari pale mvua zinapokuwa kubwa kwa kuondoka maeneo ambayo wanayaona yanaweza kuwaletea shida na kukimbilia maeneo yaliyosalama.

”Gharama ya hali mbaya ya hewa kukuta katika eneo ambalo si salama ni kubwa kuliko kuondoka kabla ya eneo hilo kuzingirwa na maji au unapoona hali ya ukame inakuwa yakupitiliza na kutafuta eneo litakaloweza kukusaidia kwa wakati muafaka,”anasema na kuongeza

”Na wenzangu ambao wanaualbinism nao wanapaswa kuchukua hatua stahiki kwa sasa kwani Jua ni kali hivyo wanapaswa kutembea na kofia ambazo zitasaidia kupunguza miozi ya jua kutokuingia katika miili yao,”anasema.

Anasema tunaelewa gharama ya lotioni kwa watu wenye ulemavu ni kubwa sana hasa zile ambazo ndio nzuri kwaajili ya kutumia kwenye ngozi,ni jambo la serikali kuona sasa ni namna gani wanaweza kusaidia ili na watu wenye ualbinism waweze kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kulinda afya zao kwa kutumia lotion ambazo ni nzuri na zenye ubora unaotakiwa.

Anasema hata kwa walemavu wasioona ni jambo la kuhakikisha nao wanazingatiwa kwa kupatiwa fimbo nyeupe ili ziweze kuwasaidia hasa kipindi cha mvua ili kujua maeneo yenye uhatarishi kuchukua hatua huku walemavu wa viungo nao kuhakikishiwa mazingira rafiki ya kupatiwa baskeli ili kuweza kukabiliana na mabadiliko haya pindi mvua inaponyesha.

Kimati anasema makundi yanayoathirika sana ni pamoja na ulemavu wa viuongo,wasione,wenye albinism ngozi inaathirika zaidi ambapo lotioni inafika kiasi cha sh.ndogo 15000 nyingine 150000 inategemea ukubwa na ubora,hawa wa viungo inabidi wapote baskeli za kutokea na wasiona wapate fimbo nyeupe.

Shaymah Nkawa Afisa Miradi kutoka Taasisi ya TCCI na Mazingira Plus anasema mabadiliko ya tabianchi ni suala mtambuka ambalo linawaadhiri binadamu kwa namna tofauti tofauti na nyanja tofauti tofauti.

Anasema binadamu anaweza kuathiriwa kutokana na maeneo yao waliyopo kutokana na maumbile yao,umri au jinsia.”Walemavu wanaathiriwa moja kwa moja kutokana na maeneo yao,ambapo asilimia kubwa walemavu wasiona viungo mfano miguu wao wanakuwa shida kubwa waliyonayo ni kushindwa kujitetea dhidi ya mabadiliko majanga ya tabianchi na pindi mafuriko yanapotokea kutoka eneo moja kwenda jingine wanaathiriwa namna ya kujiokoa.

Akitolea mfano maporomoko ya hanang anasema ni ngumu kwa mtu mwenye ulemavu wa viungo hasa wa miguu kushindwa kukimbia kujiokoa kuliko mtu ambaye yupo kawaida.

Akizungumzia walemavu wa Ngozi(Albinism)anasema kutokana na joto kali linaloongezeka sasa hivi ni namna tofauti wanavyoathiriwa kwa watu wa kawaida hivyo kusababisha kupata Kansa na kujikinga na jua kali,Mlemavu Kiziwi namna gani atakavyokabiliana na mtu ambaye anayesikia jangwa la mafuriko yanapotokea anashindwa kupiga kelele ili mtu mwingine asikie kama kuna kitu kinatokea.

***Serikali inasemaje

Makamu wa Rais ,Dkt. Philip Mpango akizungumza mkakati wa Serikali katika majadiliano ya viongozi wa juu wa mataifa mbalimbali Mwaka 2023 katika ajenda ya mabadiliko ya tabianchi katika Mkutano wa Tano wa Umoja wa Mataifa wa Nchi Zinazoendelea (LDCs) unaofanyika Doha nchini Qatar.
anatoa wito kwa mataifa kuhakikisha masuala ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi na kudhibiti uzalishaji wa gesi joto yanajumuishwa katika mipango ya maendeleo kwa kuzingatia sekta zilizo hatarini kukabiliwa na mabadiliko ya tabianchi kama vile nishati, kilimo na maji.

Anasema ni muhimu kuongeza ushirikiano wa kikanda na kimataifa katika kutafuta ufumbuzi wa changamoto zinazoyakabili mataifa kwa sasa na kuwekeza katika teknolojia bunifu zinazofaa katika kushughulikia mabadiliko ya tabianchi na changamoto zinazohusiana ili kuwa na mweleko mzuri wa baadaye.

Makamu wa Rais anasema maazimio yaliofikiwa katika mikutano iliopita ya mazingira ikiwemo ya Glasgow, Paris na Sharm El- Sheikh lazima yazingatiwe na kutoa wito wa kuzingatia haki kwa nchi za Afrika katika kuelekea katika matumizi ya nishati safi.

Akitaja athari za mbalimbali zilizoikumba Tanzania kutokana na mabadiliko ya tabianchi ikiwemo mabadiliko ya hali ya hewa kukiwa na matukio makubwa kama vile ukame na mafuriko, hali ya mvua isiyotabirika, kupanda kwa kina cha bahari na baadhi ya visiwa kuzama na kusababisha uhaba wa chakula, migogoro ya kijamii pamoja na kupanda kwa gharama za Maisha.

Anasema kwamba Tanzania inakadiriwa kuwa na hasara ya kiuchumi hadi kufikia dola milioni 33.7 katika kipindi cha miaka kumi iliyopita kutokana na mafuriko.

Makamu wa Rais anasema katika kukabiliana na hali hiyo serikali inachukua hatua mbalimbali ikiwemo uchimbaji wa mabwawa kuhifadhi maji, kuhamasisha nishati safi ya kupikia, upandaji miti kila mkoa, kujenga kingo kando ya bahati kudhibiti mmomonyoko wa udongo,mkakati wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi pamoja na kuandaa mpango kabambd wa Mazingira wa mwaka 2022-2032.

***Watu wenye Ulemavu wanasemaje juu ya mabadiliko ya tabianchi
Ally Thabiti mlemavu wa Kutoona ,anasema mabadiliko ya tabianchi nchi yamekuwa chanzo cha kurudisha Maendeleo ya Kiuchumi nyuma kwa watu wenye ulemavu kutokana na kushindwa kwenda kujitafutia fedha za kujikimu kinaisha.

Anasema imekuwa Mtihani kwao endapo mvua ikinyesha nyingi au jus kuwa Kali baadhi ya watu wenye ulemavu kushindwa kabisa kufanya shughuli mbalimbali.”Unakutwa mtu anashindwa kutoka hadi aagize usafiri endapo kama mvua Kali inanyesha au jus likiwa Kali sanaa kwa watu wenye ualbinism hivyo kuwasababisha kudidimia Kiuchumi,”anasema.

“Hatua mbalimbali zinatakiwa kuchukuliwa ili kuhakikisha Mabadiliko haya yanachukuliwa hatua na kudhibiti na Mipango mbalimbali inapaswa kupangwa ili kuhakikisha elimu stahiki inatolewa kwa makundi haya ya kuona ni namna gani wanaweza nao kuhakikisha wanakabiliana na changamoto zitokanazo na mabadiliko ya tabianchi,”anasema.

Subira Omary anasema elimu stahiki inahitajika kutolewa kwa watu wa Makundi hayo ya wenye ulemavu ili nao waingia katika mpango wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi ambayo yameathiri eneo kubwa la Dunia