Na Mwandishi wetu,Timesmajira
Mwenyekiti Bodi ya Ushauri ya Wizara kwa TMDA (MAB), Eric Shitindi amekutana na wasimamizi wa sheria mbalimbali katika kituo cha Mpaka cha Mutukula, Kagera tarehe 29 Januari, 2026 na kuteta kuhusu masuala ya udhibiti wa bidhaa za dawa na vifaa tiba katika kituo hicho.
Akizungumza na watendaji hao, Mwenyekiti amesema lengo la ziara hiyo ni kujionea shughuli za kiudhibiti maeneo ya Mpakani ba kujifunza changamoto zilizopo ili kushauri namna ya kuzitatua.
” Serikali ni moja na yote yanayofanyika yanalenga kuhudumia wananchi, hivyo rai yangu ni kuendelea kushirikiana katika kutatua changamoto za mipakani” , amesema Shitindi.

Akitoa taarifa ya utendaji wa kituo, Afisa Mfawidhi wa Kituo cha Forodha cha Mutukula, Lubinza Edmund, amesema kituo hicho kina taasisi 20 za udhibiti na jumla ya watumishi ni 116 ambao hufanya kazi kwa ushirikiano katika kubaini magendo na kukabiliana nayo ili kuhakikisha soko la Tanzania linakuwa salama kwa mujibu wa sheria zilizopo.

Lubinza ameendelea kuainisha changamoto nyingine kuwa ni ukubwa wa Mpaka ambao una vipenyo vingi, jambo ambalo ni hupelekea bidhaa kuingia kwa kificho hivyo ni lazima watendaji kushirikiana muda wote.
Ziara hiyo katika jituo cha Mutukula, iliyoongozwa na Mwenyekiti wa MAB,Eric Shitindi ilijumuisha wajumbe wote wa Bodi na Menejimenti ya TMDA ilifanyika ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yao ya Bodi.

More Stories
Dkt.Tulia,Mwalunenge waungana kutatua changamoto ya barabara
TUCASA yaomba kuanzishwa sheria malipo sekta ya ujenzi
Kihongosi:Uhai wa chama mashina