December 22, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Katibu wa Itikadi na Ueneza CCM ,Humphrey Polepole akiongea na waandishi wa habari viwanja vya Jamhuru Dodoma,

Maandalizi Uzinduzi Kampeni CCM yamekamilika

Na Penina Malundo,TimesMajira,Online

KATIBU wa Itikadi na Ueneza CCM ,Humphrey Polepole amesema maandalizi ya Uzinduzi wa Kampeni ya Chama hicho yamekamilika na ratiba kuanza rasmi saa moja asubuhi hadi 12 jioni.

Uzinduzi huo unatarajiwa kuanza kupambwa na baadhi ya wasanii mbalimbali akiongozwa na Nassibu Abdul alimaarufu kwa jina la Diamond Platinumz na Ali Salehe Kiba( Alikiba) kutoka nchini na kupamba na vibao vyao vya nyimbo za CCM.

Akizungumza leo baada ya kukamilika kwa maandalizi hayo,Polepole amesema baada ya kuaanza kwa wasanii hao kutoa burudani kuanzia saa moja mchana Rais John Magufuli atapanda jukwaani na kuwa tayari kuzungumza na wanaccm waliopo nchini na ulimwenguni.

Moja ya jukwaa litakalotumika katika uzinduzi wa kampeni ya ccm viwanja vya Jamhuri.

Amesema pia nje ya uwanja wa jamhuri tayari wamefunga Luninga kubwa kwaajili ya watu ambao hawatapata nafasi ya kuingia uwanjani endapo uwanja utakuwa umejaa.

Polepole amesema Rais Magufuli ataweza kuumbia umma juu ya miaka mitano ya uongozi wake alichokifanya na changamoto alizozipitia katika kipindi hicho.

“Dkt Magufuli atauelezea umma mambo mara tatu yake makubwa maono yake na maono ya Chama cha Mapinduzi CCM kwa watanzania na wanaccm,”amesema

Takribani majukwaa matatu yamefungwa uwanjani kwa ajili ya Uzinduzi wa kampeni ya CCM kuelekea uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 28,2020.