Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma
NAIBU Waziri wa Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wanawake na Makundi Maalum Mwanaidi Ali Khamis amewataka Maafisa Ustawi wa Jamii kuwa mabalozi wema katika maeneo yao katika kuwahudumia wananchi na kukuza ustawi wa jamii.
Naibu Waziri huyo ameyasema hayo leo Septemba 7,2023 wakati akifunga Mkutano wa siku mbili wa Maafisa Ustawi wa Jamii kutoka mikoa na Halmashauri zote nchini uliofanyika mkoani Dodoma yaliyolenga kuboresha utendaji wa maafisa Ustawi hao.
“Mheshimiwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ni mdau mzuri katika masuala ya Ustawi wa jamii na ndiyo maana alipoteuliwa tu kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akaunda Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wanawake na Makundi Maalum ,Kwa hiyo mkitoka hapa mkawe mabalozi wazuri katika kuwahudumia wananchi,
“Wizara hii ameiunda kwa sababu anajua changamoto za watanzania ,anaelewa malengo ya watanzania,anajua matatizo yanayowakabili ndiyo maana aliunda wizara hii akijua kwamba ana maafisa wake wa Ustawi wa Jamii watawahudumiwa wananchi hawa,na nyie mpo hapa katika mafunzo haya kwa ajili ya kujengeana uwezo ambao mkitoka hapa mtakuwa mabalozi wazuri katika mikoa na halmashauri zenu kuhakikisha mnawahudumia vizuri wananchi na kuona kwamba serikali na Rais wao yupo .”amesema Mwanaidi
Aidha Naibu Waziri huyo maesema,Serikali inatambua kazi inayofanywa na maafisa hao huku akisema ,itaendelea kuboresha miundombinu ya huduma na kuweka mazingira wezeshi yatakayowawezesha kufanya kazi zao kwa ufanisi.
Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia na Makundi Maalum Seif Shekalaghe amewaasa Maafisa Ustawi wa Jamii hao kuhakikisha wanakwenda kutekeleza maagizo yaliyotolewa na Makamu wa Rais Dkt.Philip Mpango wakati akifungua mkutano huo.
“Maelekezo yote yaliyotolewa mkayatafsiri na kuyawekea mkakati wa utekelezaji ,itapendekeza tunapokuja kukutana wakati mwingine tutoe taarifa ya utekelezaji wa maagizo hayo.”amesema na kuongeza kuwa
“Ndugu zangu,mengi jana yamesemwa na maelekezo,wajibu wangu na nyie pamoja na viongozi wengine wa kisekta sisi ni wa kusimamia utekelezaji wa maelekezo ya viongozi wetu.”
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu ,Ofisi ya Rais ,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Dkt. Wilson Charles amewataka Mafisa Ustawi wa Jamii hao kuhakikisha wale wote wanaobaka watoto wanawafikisha kwenye vyombo vya sheria kwa ustawi wa watoto hapa nchini.
Aidha amewataka wakurugenzi wa Halmashauri kutenga fedha kwa ajili ya watoto wanaoishi katika mazingira magumu na hatarishi ili ustawi wa Jamii uweze kusonga mbele
More Stories
Waziri Mavunde:Benki Kuu yanunua tani 2.6 za Dhahabu nchini
Kampeni msaada wa kisheria ya mama Samia kutatua kero za kisheria Katavi
Wizara ya madini yakusanya bil.521 nusu ya kwanza mwaka wa fedha 2024/25