November 6, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Maafisa kilimo watakiwa kufanya kazi kwa weredi kuleta tija

Na Israel Mwaisaka, TimesMajira Online, Rukwa

Maafisa Kilimo Wilayani Kalambo Mkoani Rukwa wametakiwa kujitathimini kwa kufanya kazi kwa weredi kutokana na baadhi yao kushindwa kutekelekeza majukumu yao kikamilifu licha ya serikali kuwapatia vitendea kazi ikiwemo pikipiki ili kuwafikia wakulima vijijini.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Wilayani humo Nichoraus Mrango kupitia kikao kazi kilicho shirikisha wataalamu wa Idara ya Kilimo, Mifugo, na Uvuvi na kufanyika katika shule ya wasichana ya Matai na kusema kila Afisa Kilimo anatakiwa kujua changamoto za wakulima na kuzifanyia kazi.

Amesema serikali ya awamu ya sita kupitia Mh,Rais wa Jamhuri ya mungano wa Tanzania  Dkt Samia Suluhu Hassan imewapatia vitendea kazi kwa maafisa kilimo ikiwemo pikipiki 59 lengo likiwa ni kuongeza uzalishaji  kwa kuwafikia wakulima wengi zaidi vijijini.

Awali akiongea kwa niaba ya Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii  Wambura Sunday aliwataka wataalam kufanya kazi kwa weredi kulingana na miongozo ya serikali ikiwemo kuwafikia wakulima kwa wakati na kutatua changamoto zao.

Hata hivyo baadhi ya maafisa mifugo wilayani humo wamesema Halmashauri ina jumla ya ng’ombe 155,010 na kwamba endapo viwanda vya kusindika maziwa vikianzishwa vitasaidia wafugaji kufuga kwa tija na kuongeza uchumi wao kutokana na wilaya hiyo kuzalisha maziwa zaidi ya lita elfu therathini kila mwezi.