Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Wauzaji wa nguo za kike na kiume Men Destination wamefungua duka jipya la nguo za kiume lengo ikiwa ni kutekelezeka maoni ya wateja wao ya uhitaji wa suti zenye ubora hasa za uturuki na nchi zingine
Mbali na uzinduzi huo, Men Destination wametoa ofa kwa Mteja wao ambaye atakayefika dukani hapo na kununua suti 1 atapata ofa ya Mafuta ya Lita 5 na atakayenunua suti 2 atapata ofa ya Mafuta ya Lita 10
Akizungumza na waandishi wa Habari juzi Jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa duka hilo lililopo posta Jijini Dar es Salaam Mmiliki wa Men Destination, Abdul Rauf alisema mbali na zawadi hizo kwa mteja, Wana huduma zilizo Bora ikiwemo uwepo wa free WiFi kwa wateja wote lakini pia huduma ya usamabaji wa bidhaa zao.
“Tumekutana na maoni mbalimbali ya wateja ikiwemo uhitaji wa suti za nchi zingine ukiachana na uturuki ambazo ziko sasa dukani, tumeanza na suti kutoka uturuki na baadae tutachanganya tutaenda na Italy”
“Tumeendelea kuwa juu zaidi hasa kubadilisha muonekano wa duka, tumejarbu kuja kwa utofauti na kuwa kama ofisi zingine nzuri”
Alisema wameamua kumtumia msanii wa bongo movie na muziki wa bongo Flave, luluDiva kuwa Balozi wao kwani anaushawishi wa hali ya juu hasa katika kutafuta wateja ambapo hadi sasa tangu waanze kufanya nae kazi wa mda mfupi mrejesho ni mkubwa.
“Balozi wetu anajitahidi sana kwenye kujiongeza, muonyeshe tu bidhaa maneno atayatoa yeye mwenyewe, ndiyo maana tukampeleka nje ili akajionee wanavyochagua mzigo, thamani ya mzigo waliokuja nao na vitu vingi zaidi “
“Kwa wiki mbili hizi tumepata muitikio mzuri wateja wameingia wengi wamependa bidhaa zetu na hadi sasa baadhi ya bidhaa zetu zimeisha ” Alisema Rauf
Kwa upande wake Balozi wa Duka hilo, LuluDiva alisema anauelewa mkubwa kuhusiana na vitu vyote vilivyopo kwenye duka hilo na wanahakikishia mteja kwamba atapata vitu vizuri vinavyoendana na ubora anaohitaji.
“Nawakaribisha wateja wetu ndani ya Men Destination kujipatia bidhaa zenye ubora wa hali ya juu”
luluDiva amewashukuru Men Destination kwa kumchagua kuendelea kuwa Balozi wao na kutangaza biashara yao.
More Stories
Startimes yazindua makala ya China, Africa
Mwanasheria wa Katavi aliyetimkia kwenye muziki achaguliwa tuzo za MIEMMA
Coca-cola ‘Kitaa Food Fest’ yahitimishwa kwa mafanikio