Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online, Mwanza
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi(CCM)Wilaya ya Nyamagana Yusuph Ludimo ni miongoni mwa makada wa chama hicho waliojitokeza kuchukua, kurejesha na kujitokeza katika usaili wa nafasi ya Uenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Mwanza baada ya aliyekuwa Mwenyekiti kuteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara Sixbert Reuben.
Chama Cha Mapinduzi kilitangaza uchukuaji wa fomu kuanzia Novemba 12 hadi 16 na siku ya Jumatatu Novemba 20, 2023 ilitangazwa kuwa ndio siku maalum kwaajili ya usaili wa makada waliochukua na kurejesha fomu kwa nafasi hiyo ngazi ya Mkoa zoezi lililoendeshwa katika ukumbi wa BOT mkoani Mwanza.
Makada wengine waliojitokeza katika kinyang’anyiro hicho ni pamoja na Dkt.Antony Dialo aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mwanza, Nelson Mesha aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilemela, Chacha Boroi, Mjumbe wa Kamati ya Siasa Mkoa wa Mwanza John Nzilanyingi, Mjumbe wa Kamati ya Siasa Elizabeth Nyingi, Mwenyekiti wa sasa wa CCM Wilaya ya Misungwi, Mwenyekiti wa sasa wa CCM Wilaya ya Ukerewe, Mwenyekiti wa sasa wa CCM Wilaya ya Sengerema na wengineo.
Yusuph Ludimo aliwahi kuwa Katibu wa kwanza wa Shirikisho la Vyuo Vikuu(SENETI) Mkoa wa Mwanza, Katibu wa CCM tawi la Kambarage Chuo Kikuu cha SAUT Mwanza, Kaimu Katibu wa uhamasishaji na chipukizi UVCCM Mkoa wa Mwanza, Mjumbe wa mkutano mkuu wa CCM Taifa, Mgombea wa nafasi ya mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Nyamagana 2017.
Pia Mbunge wa Serikali ya wanafunzi chuo kikuu cha SAUT Mwanza, Rais wa Serikali ya wanafunzi shule ya sekondari Turiani, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Nyamagana, Katibu wa UVCCM tawi la Muhalitani na mwenyekiti wa shina la wakereketwa Harakati.
More Stories
Prof. Mwakalila asisitiza uadilifu, uzalendo kwa wanafunzi wapya chuo cha kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere
Benki ya Equity Tanzania yasaini mkataba wa kuwawezesha wanawake kiuchumi
Rais Samia alivyoguswa kifo cha msanii Grace Mapunda