Na David John,TimesMajira Online, Ludewa,
WANANCHI wa Ludewa mjini mkoani Njombe kwa pamoja wamekubaliana kumchagua Mgombea Udiwani kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kata ya Ludewa Mjini Monica Mchilo, kwa kudai kuwa mgombea huyo anatosha na bado wanaimani nayo.
Wanadai mgombea huyo, katika kipindi chote Cha uongozi wake huko nyuma amefanya mambo makubwa kwa ajili ya wananchi wa Ludewa, hivyo hawaoni sababu ya kuacha kumchagua tena ili aendelee kuchapa kazi kwa kushirikiana na Mbunge wa Jimbo hilo Josepha Kamonga ambaye amepita bila kupingwa.
Wameyasema hayo leo wilayani hapa kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea huyo uliofanyika katika viwanja vya Mariam Keeja Ludewa Mjini. Wamesema kwa kazi kubwa alizofanya Mchilo hawaoni sababu ya kubadilisha na badala yake watachagua mafiga matatu ili kumrahisishia kazi Rais Dkt John Magufuli.
“Nataka niwaombe wananchi wezangu mimi binafsi namjua vizuri mamam huyu. ni mwaminifu na mwadilifu sana na kwa uchapakazi wake hakuna mashaka kabisa hivyo nawaomba tumchague kwa Kura nyingi Sana,” amesema Maiko Mwinuka
Amesema, anawaomba wananchi wote wa kata ya Ludewa mjini kuepuka maneno maneno ya wapinzani ambayo kimsingi hayana maana yoyote kazi yao ni matusi tu na si maendeleo, hivyo wao kama wananchi wa kata ya Ludewa mjini wanahakikisha wanampa Monica kura zote.
Naye Johanes Komba amesema, Mgombea huyo wa CCM anafaa na katika kipindi chake Cha uongozi, amekuwa mtu sahihi na ni msaada mkubwa kwa wananchi wa Ludewa hususani kata ya Ludewa mjini.
Kwaupande wake Basir Makungu katibu wa elimu Mazingira na maadili ndani ya Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Ludewa, amewataka wananchi kuacha kufanya makosa na wasidanganywe na wapinzani kwani hawana jipya.
Amesema, Chama Cha Mapinduzi (CCM), kinaongea kwa takwimu na si porojo na hata wananchi wenyewe wanalijua hilo, hivyo nivyema wakaendelea kuiamini CCM.
Kwaupande wake mgombea udiwani wa Chama hicho kata ya Ludewa mjini Monica Mchilo alitumia mkutano huo kuwahutubia wananchi kwamba waendelee kumwamini na katika kipindi chake amefanikiwa kufanya mambo mengi makubwa .
“Ndugu zangu wananchi naombeni kura zenu. Kama mnavyojua Mwezi huu Oktoba 28 tunafanya uchaguzi mkuu niwaombe msifanye makosa kura zote kwa CCM, mumchague Rais Dkt. John Magufuli na Mimi Monica Mchilo Kama Diwani wenu,”amesema Monica
Pia katika mkutano huo alitoa ufafanuzi juu ya utekelezaji wa miradi mbalimbali yanayotokana na fedha za Halmashauri pamoja na zile ambazo zinatoka serikali kuu kusaidiana na wananchi, hivyo ili kuendeleza kazi wahakikishe wanachagua Chama Cha Mapinduzi (CCM)Na David John Ludewa
WANANCHI wa Wilaya ya Ludewa mjini mkoani Njombe kwa pamoja wamekubaliana kumchagua Mgombea Udiwani kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi CCM kata ya Ludewa Mjini Monica Mchilo kwa kudai kuwa mgombea huyo anatosha na bado wanaimani nayo sana.
Wamesema kuwa mgombea huyo wa udiwani katika kipindi chote Cha uongozi wake huko nyuma amefanya mambo makubwa kwa ajili ya wananchi wa Ludewa mjini hivyo hawaoni sababu ya kuacha kumchagua ili akaendelee kuchapa kazi kwa kushirikiana na Mbunge wa Jimbo hilo Josepha Kamonga ambaye amepita bila kupingwa.
Wananchi hao wameyasema hayo leo wilayani hapa kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea huyo uliofanyika katika viwanja vya Mariam Keeja Ludewa Mjini. Ambapo wamesema kuwa kwa kazi kubwa alizofanya Mama Mchilo hawaoni sababu ya kubadilisha na badala yake watachagua mafiga matatu ili kumrahisishia kazi Rais Dkt John Magufuli..
“Nataka niwaombe wananchi wezangu Mimi binafsi namjua vizuri mamam huyu .ni mwaminifu na mwadilifu Sana na kwa uchapakazi wake hakuna mashaka kabisa hivyo nawaomba tumchague kwa Kura nyingi Sana.”amesema Maiko Mwinuka
Amesema kuwa anawaomba wananchi wote wa kata ya Ludewa mjini kuepuka Maneno Maneno ya wapinzani ambayo kimsingi hayana maana yoyote kazi yao ni matusi tu na si Maendeleo hivyo wao Kama wananchi wa kata ya Ludewa mjini wanahakikisha wanampa Monica .
“Nawaomba wananchi wezangu kuchagua mafiga matatu na kikubwa lazima mheshiwa Rais wetu apate mtu wa kufanya naye kazi Sasa Kama tutachanganya atakosa mtu sahihi “ameongeza Nuthurupia Haule.
Naye Johanes Komba amesema Mgombea huyo wa CCM anafaa na katika kipindi chake Cha uongozi wake wa awamu mbili za uongozi wake Mara zote amekuwa mtu sahihi na ni msaada mkubwa kwa wananchi wa Ludewa hususani kata ya Ludewa mjini.
Kwaupande wake Basir Makungu katibu wa elimu Mazingira na maadili ndani ya Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Ludewa amewataka wananchi kuacha kufanya makosa na wasidanganywe na wapinzani kwani hawana jipya.
Amesema kuwa chama Cha Mapinduzi kinaongea kwa takwimu na si porojo na hata wananchi wenyewe wanalijua hilo .hivyo nivema wakaendelea kukiamini Chama Cha Mapinduzi CCM.
Kwaupande wake mgombea udiwani wa Chama hicho kata ya Ludewa mjini Monica Mchilo alitumia mkutano huo kuwahutubia wananchi kwamba waendelee kumwamini na kwamba katika kipindi chake amenikiwa kufanya mambo mengi makubwa.
“Ndugu zangu wananchi nipo.mbeleni yenu kuomba kura zenu .Kama mnavyojua Mwezi huu Oktoba 28 tunafanya uchaguzi mkuu niwaombe msifanye makosa kura zote kwa ccm .mumchague Rais Dkt. John Magufuli na Mimi Monica Mchilo Kama Diwani wenu,”amesema Monica
Pia katika mkutano huo alitoa ufafanuzi juu ya utekelezaji wa miradi mbalimbali yanayotokana na fedha za Halmashauri pamoja na zile ambazo zinatoka serikali kuu kusaidiana na wananchi hivyo ili kuendeleza kazi wahakikishe wanachagua Chama Cha Mapinduzi CCM.
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa