Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Mwaka wa pili mfululizo, LSF imeshiriki na kuwezesha Kongamano la Kitaifa la Wanawake lenye lengo la kujadili tafiti mbalimbali zilizofanyika katika masuala ya wanawake ili kubaini hali halisi na kuweka mipango mikakati katika kushughulikia masuala ya wanawake katika nyanja ya kiuchumi, kijamii, na kisiaasa kwa ajili ya kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Akizungumza wakati wa kongamano hilo, Meneja Rasilimali na Mawasiliano LSF, Jane Matinde amesema Haki Yangu App itasaidia kuendana na ubunifu wa teknolojia na kuwawezesha wanawake na wasichana kijamii na kiuchumi lakini pia kuhakikisha huduma za msaada wa kisheria na upatikanaji wa haki kwa wote.
“Katika kuendana na ubunifu wa teknolojia ili kuwawezesha wanawake na wasichana kijamii na kiuchumi na kuhakikisha huduma za msaada wa kisheria na upatikanaji wa haki kwa wote, LSF tumezindua Haki Yangu App inayowezesha kupata elimu ya kisheria, kupata huduma za msaada wa kisheria , kutoa mafunzo maalumu kwa wasaidizi wa kisheria. Kupitia Haki Yangu App, kesi takribani 315 zikiwemo za unyanyasaji wa kijinsia, migogoro ya ardhi, mirathi, migogoro ya ndoa, matunzo kwa watoto zimeripotiwa na kufanyiwa kazi.” Amesema Matinde
More Stories
Puma Energy Tanzania yampongeza Rais Samia kwa mazingira mazuri ya uwekezaji, yang’ara tuzo za TRA
CHAMUITA wamtunuku Tuzo Msama
‘Valentine day’kutumika kutangaza mapango ya Amboni