Na Agnes Alcardo, Timesmajira Online
UONGOZI wa Lizy Park umeandaa tamasha maalum linalolenga kusaidia watoto yatima na wazee wasiyojiweza, kwa kushirikisha bendi nne zitakazotumbuiza usiku wa Aprili 25, 2025 katika ‘Kiota’ cha Lizy Park kilichopo maeneo ya Sinza Lion zamani pakijulikana kama T Galden.
Kati ya bendi hizo zitazotumbuiza ni pamoja na bendi ya RTS (Kihangaiko), Ruvu Star’s, Mbweni JKT na Sikinde OG,huku mshindi wa kwanza ataondoka na zawadi ya kiasi cha milioni 2, wa pili milioni 1 na watatu 500,000.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar-es -Salaam, Mkurugenzi wa Lizy Park, Elizabeth Chacha, amesema, lengo la kuandaa tamasha hilo ni kurudisha kwa jamii,ambapo kiasi kitakachopatikana kwenye tamasha hilo chote kitapelekwa kwa wahitaji hao.
“Wapo watu wengi wenye uhitaji, hivyo Lizy Park tumeona ni vyema kupitia sherehe hizi ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar tukaadhimisha kwa kujitolea kwa jamii yenye uhitaji,” amesema Elizabeth.
Kwa upande wake Mratibu wa Tamasha hilo, Cecilia Jeremiah, ametoa wito kwa wadau wa muziki wa dansi kuhudhuria kwa wingi, ili kuunga mkono juhudi hizo ikiwa pamoja na kupata burudani kutoka kwa magwiji hao.
More Stories
Rais Samia :Kadiri nchi inavyofunguka ndivyo inavyohitaji mabadiliko ya sheria
Rais Samia ashiriki mkutano wa kimataifa wa mabadiliko ya tabianchi kwa njia ya mtandao
Benki ya Exim yakabidhi madarasa kwa shule mbili za sekondari Kigoma