January 8, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Linkee, programu mpya ya usafiri, yaanza mchakato wa usajili

Na Mwandishi wetu, TimesMajira online

Linkee, kampuni mpya ya kiteknolojia yatangaza mchakato wake wa usajili wa madereva Dar es Salaam na kuwakaribisha madereva wote kujiunga mapema kwenye programu yao ili kufurahia faida nyingi za kipekee. Mwaliko huu ni kwa ajili ya madereva wa magari, pikipiki na bajaji. Linkee inajiandaa kufanya uzinduzi wake jijini Dar es Salaam, ambapo kampuni hii mpya inalengo la kufanya mapinduzi kwenye ujasiriamali, usafiri na katika uchumi wa kugawana.


Kutokana na kwamba Dar es Salaam ni soko la uzinduzi la kampuni hii, Linkee inataka kutengeneza muamko wa nguvu kwa madereva kupitia nafasi hii ya kipekee kwenye soko ya kutoa mapato yote kwa miezi 6 baada ya uzinduzi kwa ajili ya madereva waliojisajili kwenye programu. Hakuna pingamizi au vizuizi au idadi ya safari zinazohitajika. Mpango huu utawahamasisha madereva kutumia Linkee, wakijua ya kuwa asilimia 100 ya faida kutoka kwenye safari zao itaenda mfukoni mwao.


Faida yote itaenda kwa madereva ambapo Linkee itatoa orodha ya safari na bei ambayo madereva watachagua kutokana na mipango yao. Linkee haitaomba idadi fulani ya safari kufanyika ndani ya siku au masaa ya kufanya kazi kwenye hii programu na haitatoa adhabu kwa dereva pale ambapo muafaka hautopatikana. Madereva wana uamuzi wa  jinsi ya kutengeneza faida zao.


Timu ya Linkee yenye jukumu la kutengeneza fursa hiyo imesherehekea hatua hii muhimu: Wana fahari kubwa kuitambulisha Linkee kwa ulimwengu mzima kupitia uzinduzi ujao jijini Dar es Salaam. Wanaleta Linkee Tanzania kwa ajili ya Watanzania, na wanaamini ahadi yao ya kuboresha mapato ya madereva na kujenga jamii ya kugawana na usafiri wa kirafiki, wenye ufanisi na rahisi ni njia sahihi kwa kampuni ya Linkee. kila senti itahesabika kwa ajili ya madereva na watumiaji wengine na pia tunaamini sasa ni wakati wa teknolojia kupatikana kirahisi ili kuboresha jamii na kukuza ubora wa maisha wa kila mmoja. “Hilo ndilo lengo la Linkee”.


Linkee itakuwa na program ya usalama  ambapo kila safari itatoa huduma ya usalama ili madereva na watumiaji waweze kutuma safari zao kwa watu wanao waamini na kama kuna uhitaji wanaweza kutoa taarifa polisi moja kwa moja. Linkee inataka kusherekea umoja na mshikamano  kupitia program hii na kutathmini safari ili watumiaji waweze kusoma maoni, mapendekezo na maswali.

Jinsi ya kujiandikisha na Linkee
Ni programu rafiki na rahisi. Na vifuatavyo ni vitu 6 ambavyo madereva wanatakiwa kupakia kwenye programu ya Linkee moja kwa moja:

Madereva:

1.- Leseni ya udereva

2.- Picha ya Wasifu

3.- Picha ya uthibitisho wa kitambulisho

Magari:

4.- Usajili wa gari

5.- Bima ya gari

6.- Picha ya uthibitisho wa gari