Na Bakari Lulela, Times Majira Online
MSANII chipukizi wa muziki wa laga Revocatus Manyota maarufu kama ‘Level star’ ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wake ‘Kifo cha Mende amesema, anatamani kufanya vizuri zaidi pale atakapopata mtu wa kumshika mkono kwani anaamini ana kipaji cha hali ya juu katika tasna ya muziki hapa nchini.
Level Star, mwenye makazi yake Temeke jijini Dar es Salaam ameonesha uwezo mkubwa katika tasnia hiyo huku kibao chake kipya kikitamba katika vituo mbalimbali vya Television.
Akizungumza na majira Level Stars amesema, miongoni mwa vibao vyake alivyowahi kuvitunga ni pamoja na Jidekeze, Umeondoka, Bolibo na Kifo cha mende ambapo amefanikiwa kurekodi video zake mbili zilizotokana na fedha za kuungaunga.
Chipukizi huyo amesema, ana ndoto ya kufanya makubwa kupitia muziki wa laga huku lengo lake ni kuelimisha na kuburudisha na amekuwa akizikubali kazi msanii maarufu nchini Diamond Platnum na kusema asilimia kubwa amekuwa akimvutia jambo lililochangia kuingia kwenye muziki.
“Navutiwa sana na msanii Diamond Platnum mbali na mafanikio makubwa aliyokuwa nayo, ameweza kuondoa sumu zilizokuwa zikijengeka vichwani mwa wazazi wangu ambapo walikuwa wakiona muziki ni kazi ya kihuni lakini hivi sasa wananihimiza nifanye jitihada ili niweze kufanikiwa,” amesema chipukizi huyo
Levo Star amesema, hivi sasa yupo radhi kushirikiana na nyota huyo na mwingine ili kuendeleza na kudumisha tasnia ya mziki hapa nchini.Chipukizi huyo amewataka wapenzi wa muziki kufuatilia nyimbo zake kupitia ukurasa wake wa Instragram na Youtube.
More Stories
GETHSEMANE GROUP KINONDONI yaja na wimbo wa siku yetu kwaajili ya harusi
Startimes yazindua makala ya China, Africa
Mwanasheria wa Katavi aliyetimkia kwenye muziki achaguliwa tuzo za MIEMMA