Na Jackline Martin, TimesMajira Online
LATRA imerejesha huduma za usafiri kwa mabasi sita ya kampuni ya Katarama Luxury kati ya mabasi 10 yaliyositishiwa leseni.
Uamuzi huo umekuja baada ya uchunguzi wa awali uliofanyika na Mamlaka hiyo kwa kushiriikiana na jeshi la polisi kubaini magari manne ya kampuni hiyo kuchezea mfumo wa VTS.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar r es Salaam , Salum pazi amesema baada ya kusitisha leseni ya kampuni hiyo , uchunguzi ulifanyika na kubaini mabasi sita hayakuingilia mfumo wa VTS.
“LATRA ilisitisha leseni za mabasi yote 10 ya Kampuni ya Katarama Luxury kwa kipindi kisichojulikana kuanzia tarehe 13 Septemba mwama huu 2024 na hiyo ilikuwa ni kwa mujibu wa kanuni ya 27 (d) na 27 (2) ya kanuni za leseni za usafirishaji kwa magari ya abiria.
“Hatua hiyo ilifuatia uchunguzi wa awali uliofanyika na kubaini kosa la kuingilia mfumo wa kufuatilia mwenendo wa mabasi kwa niia ya kubadili sehemu ya kifaa cha kufatilia mwenendo wa mabasi kwa kuweka kifaa kingine kinachosababisha utumaji wa taarifa potofu katika mfumo wa VTS”
Hata hivyo amesema jeshi la polisi linaendelea kufanya uchunguzi kwa mabasi manne yaliyobakia ikiwemo basi lenye usajili namba T 420 EBR ,T836 EBR , T835 EBR na T 485 DXP.
Hata hivyo amesema mabasi sita yaliyo ruhusiwa kutoa huduma ni yale yanayofanya safari zake DAR -Mwanza, na Dar Bukoba.
Aidha Pazi amesema mamlaka inaendelea kufualitilia mienendo ya wasafirishaji huku akisisitiza kuwa haitosita kuchukua hatua kali itakapo baini ukiukwaji wa masharti ya leseni ya usafirishaji.
“Mamlaka inawashukuru wasafirishaji ambao wanaendelea kutoa huduma kwa ufanisi bila kukiuka sheria, utaratibu na kanuni za nchi hii na pia mamlaka inaendelea kuwakumbusha wasafirishaji wote kwamba inaendelea kufatilia magari yote yanayotoa huduma na yaliyopewa leseni kwa mujibu wa sheria na itakapobainika uvunjifu wa sheria, taratibu na kanuni au hila za aina yoyote za kuharibu utaratibu uliowekwa kwa mujibu wa sheria ambao unapelekea kusababisha hasara ambazo hazikuhitajika, mamlaka haitosita kuchukua hatua”
Kwa upande wake wake Mkuregenzi wa kampuni hiyo Lauriani Katarama katarama -ameahidi kuzingatia sheria za leseni za usafishaji kama inavyoelekezwa ma mamlaka.
“Nimepokea masharti ya LATRA waliyonipa, naahidi kuyatimiza na kusafirisha abiria bila kuwa na changamoto yoyote mpaka mwisho wa kituo, nawashukuru sana kwa kunirejeshea magari yangu sita naomba wateja wangu wawe na imani na mimi katika safari tunayoendelea nayo”
“Naomba radhi kwa abilia ambaye amepata changamoto kwa wale waliokuwa wamekata tiketi za usafiri kwa kutopata huduma za magari yetu n tunawaahidi kuwasafirisha salama” Aliongeza
More Stories
RC Mrindoko:Vyombo vya haki jinai shirikianeni kumaliza kesi kwa wakati
RC Katavi ataka huduma ya maji safi na salama iimarishwe kudhibiti Kipindupindu
Walengwa TASAF Korogwe TC watakiwa kuchangamkia fursa