November 8, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

LATRA yaja na marekebisho ya sheria zake mbili

Na Joyce Kasiki,Timesmajira online

KAIMU Mkurugenzi wa Huduma za Sheria wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) Mwadawa Sultan  ametambulisha sheria mbili ambazo zinaenda kufanyiwa marekebisho ili kuwezesha utekelezaji 

“Kimsingi tumeona changamoto zipo katika utekelezaji wa sheria ndio maana tumeleta mapendekezo ya marekebisho ya sheria ili iweze kutekelezeka.”amesema Sultan

Sultan ameyasema hayo katika Jengo la LATRA kwenye maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa jijini Dar Es Salaam huku alitaka sheria hizo zinazoenda kufanyiwa marekebisho kuwa ni Sheria ya LATRA Sura Na.413 na sheria ya leseni za usafirishaji ya 1973 Sura Na.317.

Vile vile amesema kanuni za sheria hizo nazo zinaenda kufanyiwa marekebisho ambapo kwa upande wa sheria ya leseni za usafirishaji matarajio ni kufanya marekebisho katika kanuni zote mbili za sheria hizo ambapo marekebisho yamegusa maeneo mengi hususan katika eneo la usafirishaji watoto shuleni ambapo masuala yote ya mabasi ya shule yatahamishiwa katika kanuni nyingine.

Kwa upande wa sheria za usafirishaji sura Na 317 zipo kanuni mbili ambazo ni kanuni ya usafirishaji wa usafiri wa Umma ya 2020 na kanuni ambayo ipo katika leseni za usafirishaji sura Na.417 amesema,kanuni hizo zimefanyiwa marekebisho makubwa ikiwemo kutoa baadhi ya huduma zilizodhibitiwa chini ya kanuni hizi kwenda kwenye kanuni nyingine.

“Mfano usafirishaji wa watoto shuleni inaenda kwenye kanuni ya usafiri wa kukodisha ,lakini maboredho mengine ni namna ya kutoa adhabu ambazo sasa zitatolewa kulingana na ukubwa wa chombo na huduma ambayo mtu anafanya,

“Katika kanuni zetu zilizopo sasa nadhani ni za aina moja ambapo vyombo vidogo vimelenga malalamiko kwamba inakuwaje wote hao watoe adhabu moja,nahi tumeangalia tumeona kweli changamoto hiyo ipo ,na kwa kuwa kazi yetu ni kuboresha huduma tumeona ipo haja ya kufanya marekebisho hapo .”

Katika kanuni za usafirishaji Sura Na.417 na kanuni za usafirishaji mizigo nazo pia zilizotengenezwa 2020 pia yapo maeneo yamerekebishwa kutokana na kero mbalimbali zilizokuwepo.

Katika eneo hilo Sultan amezungumzia adhabu zitolewazo katika maguta ambayo yapo chini ya tani moja adhabu zake zipo sawa na maguta ya tani 10 na kuendelea na hivyo LATRA ikaona ipo ya kufanya marekebisho na imeendaa mapendekezo.

“Kwa ujumla,mapendekezo yote yalipelekwa kwa katika kikao cha wadau Mei 2024 na tumepokea maoni yao “

Katika hatua nyingine amesema katika marekebisho hayo hivi sasa LATRA inatumia mawakala walioidhinishwa na Mamlaka katika usafiri wa kukodisha ambapo jukumu lao ni kukatisha leseni za Mamlaka kwa niaba yake .

Sultan lisema,LATRA imeendaa utaratibu maalum wa kutekeleza shughuli za mawakala hao huku akisema kipindi cha nyuma kazi hiyo ilifanywa na halmashauri.