Na Penina Malundo,timesmajira, Online
WATANZANIA wametakiwa kutumia fursa mbalimbali za kibiashara zinazojitokeza katika nchi ya Iran.Â
Wito huo umetolewa jana na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (Tantrade), Latifa Khamis wakati wa maadhimisho ya Iran Day yaliyofanyika katika viwanja vya maonesho ya Kimataifa ya biashara (Sabasaba).
Amesema lengo la kuja na siku hiyo ambayo ni ya kwanza katika maonesho hayo ya 46 yanayoendelea, ni kuadhimisha mahusiano ya Tanzania na Iran ambayo ni ya miaka 40 sasa.
“Pia tumeamua kuadhimisha siku hii ya Iran kwasababu tunatilia mkazo fursa baina ya nchi hizi mbili. Tumeona tusitumie maonesho haya kwa kutembelea na kuona tu, bali kuudumisha kwa misingi ya kibiashara katika majukumu yetu yanayotukabili kila siku kuhakikisha nchi zetu kila mmoja anatumia fursa ya mwenzie katika kuendelea biashara.
“Kwahiyo nitoe wito kwa watanzania kuweza kutumia fursa mbalimbali zinazojitokeza katika nchi hii. Na siku hii ya leo tunawaita ili kuamsha zile fursa ambazo hatujazitumia baina yetu,” amesema Latifa.Â
Amebainisha kuwa, baada hapo wataweza kufanya misafara ya kibiashara na kuona kitu wataweza kufanya kwa kuanzia, pamoja na kuhamasisha biashara baina ya nchi hizo mbili.
Amesema ziara hiyo Iran imelenga kuonesha fursa zilizopo kwao ambazo kwa nchi yetu tunaweza kuzitumia katika maeneo mbalimbali.Â
“Kupitia fursa za Iran sisi tunazifanya kimkakati zaidi, Tanzania tunafanya diplomasia ya uchumi, hivyo tuko hapa kutokana na kazi kubwa aliyofanya Rais Samia kuhamasisha mambo mbalimbali. Kwa mara ya kwanza tuna siku hii ya Iran Day katika maonesho haya, na ni mwanzo tu…kutakuwa na misafara mingi baina yao ambayo italeta tija” amesisitiza.
Naye Kaimu Balozi wa Iran, Hussein Bahineh amesema Nchi ya Iran imejikita katika uwekezaji hasa sekta ya gesi, madini, Teknolojia kwasababu wenzetu tumeona ni wataalam mbalimbali .
“Tunafurahi kuwepo katika maonesho haya kusherekea ushirikiano wetu uliodumu muda wa miaka 40, na tutaendeleakushirikianana Tanzania katika mambo mbalimbali, “amesema Bahineh.
More Stories
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba
TRA kuongeza idadi ya waendesha uchumi walioidhinishwa
TRA Tanga wajivunia ukusanyaji mapato