Na Zena Mohamed,Timesmajiraonline,Dodoma.
MKURUGENZI Mkazi wa Shirika la kutetea umiliki wa ardhi Tanzania (LANDESA), Dkt.Monica Mhoja ameiasa jamii kuachana na mila kandamizi ambazo zimekuwa zikiwapa nguvu kubwa watoto wa kiume katika ngazi ya familia jambo ambalo linamfanya mwanaume awe na maamuzi ya moja kwa moja kwenye haki ya umiliki wa Ardhi kuliko mwanamke.
Amesema kulingana na haki za umiliki wa Ardhi ni makosa kwa mwanaume kuwa muamuzi pekee katika masuala ya ardhi.
Kutokana na kuonekana kuwa wanaume wamekua wakiwa na maamuzi zaidi kuliko wanawake LANDESA imeshiriki mkutano wa Kimataifa wa kuangalia Kamisheni ya hali za watu Duniani uliofanyika nchini Marekani kwa njia ya Mtandao kujadili haki za Ardhi kwa Mwanamke hususani katika kushirikishwa katika matumizi ya Ardhi.
Akizungumza katika mkutano huo Mkurugenzi mkuu wa Shirika la LANDESA Tanzania
Dkt.Monica Mhoja ,amesema kuwa Shirika hilo limejikita katika kuangalia haki za masuala ya ardhi,usalama wa Ardhi kwa wananchi hasa kwa wale wanaoishi vijijini.
Ameeleza kuwa Shirika la LANDESA ni la kimataifa ambalo limeanzishwa mwaka 1981 na kwa hapa Tanzania limesajiliwa chini ya sheria za Asasi zisizo za Kiserikali katika kutete haki za Ardhi na matumizi yake.
“Wanawake katika nchi zinazoendelea kama Tanzania wanabeba kwa kiasi kikubwa athari za mabadiliko ya tabianchi kwa sababu ya maisha yao ya kutegemea ardhi na maliasili na ripoti zimetuonyesha kuwa shughuli za ardhi na matumizi huchangia jumla ya utoaji wa kaboni lakini kwa upande mwingine suluhu za ardhi ambazo zinawahusisha wanawake huchangia katika kukabiliana na changamoto za uhaba wa chakula na uharibifu wa ardhi kutokana na mabadiliko ya tabianchi,”amesema
Ameongeza kuwa kutokana na mkutano wa 66 wa Kamisheni ya hali ya watu uliofunguliwa march 14 ambao utafikia mwisho Machi 25 mwaka huu ,hivyo wao Kama Shirika la LANDESA kwa kushirikiana na Oxfam na landesa Tanzania waliamua kushiriki mkutani huo pembezoni ili kujadili kwa kina jinsi wanawake wanavyochukua uongozi katika mapambano dhidi ya janga la hali ya hewa Duniani kote.
Aidha Shirika hilo limeendelea kufuatilia matukio mbalimbali yahusuyo haki za Ardhi na matumizi yake hasa kwa makundi mbalimbali wakiwepo vijana ,Wanawake na Watu wenye ulemavu wanahusishwa kwa namna gani katika kutoa maamuzi ya kumiliki na kutumia Ardhi kwa haki na usawa.
Hata hivyo amewataka wanawake wote nchini kutojidharau na kujiona wanyonge katika kushiriki shughuli mbalimbali katika jamii inayowazunguka na hali hiyo itawapelekea kujiamini na kushiriki katika ngazi mbalimbali ya maamuzi katika ngazi zote hasa masuala ya haki ya kumili ardhi.
Kwa upande wa wake Afisa Maendeleo ya Jamii Mwandamizi Bi.Rennie Gondwe kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia wanawake na Makundi Maalum alisema kwa sasa serikali imeweka maafisa Maendeleo ya Jamii kila ngazi kuanzia ngazi ya Taifa hadi Mtaa jambo ambalo limesaidia kwa kiasi kikubwa wananchi hasa wanawake kupata haki zao kwa haraka bila kusumbuliwa.
“Tunaona kwa sasa kumekuwa na mabadiliko makubwa ukilinganisha na miaka ya nyuma ambapo kwa sasa Mwanamke anahusishwa na kusimamia moja kwa moja katika ngazi zote za maamuzi hapa nchini Tanzania,”amesema.
More Stories
Rais Samia afurahia usimamizi mzuri wa miradi
Rais Samia apongezwa kwa kuboresha huduma kwa wazee
Watu 5,000 kuhudhuria tamasha la utamaduni Songea