January 8, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Simba jike husihi zaidi kuliko simba dume. (Picha ya Mtandao)

KWA TAARIFA YAKO: Ukiacha binadamu pia Simba jike anaishi muda mrefu kuliko dume

Na Mwandishi Wetu,

Karibu dunia nzima inaaminika mwanamke anaishi muda mrefu kuliko mwanaume, lakini kwa taarifa yako tu jambo hili sio kwa mwanadamu pekee, bali hata baadhi ya Wanyama hali ni kama hiyo.

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na kuchapishwa na mtandao wa Sciencing.com, simba ni kati ya Wanyama ambao majike ya simba yanaweza kuishi muda mrefu zaidi mpaka zaidi ya asilimia 50 ya maisha ya madume.

Sababu ni pana sana. Moja ya sababu hizo ni kwamba majike hujichanganya zaidi kuliko madume au kwa maneno mengine, madume muda mwingi ni mapweke. Ambapo majike hujichanganya na kushirikiana kwa kiasi kikubwa kwenye kuwinda, kulea watoto lakini pia kunafaida ya kujichanganya.

Madume hupunguza muda wa kuishi sababu ya jukumu lao na umuhimu wa kulinda zaidi haswa katika vitisho mbalimbali ikiwepo shughuli za kibinadamu ambazo huwa ni tishio kwenye maisha yao. Shuguli hizo ni pamoja na kuwinda ambapo binadamu hulenga kuua madume makubwa, ambapo kwa kufanya hivyo muwindaji hujizolea sifa.