November 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Faru Najin akiwa amepumzika mbugani nchini Kenya. (picha na Natgeo)

KWA TAARIFA YAKO: Aina hii ya faru wamebaki wawili tu ulimwenguni

Na Mwandishi Wetu

KIFARU aitwaye Najin, pichani yuko nchini Kenya aliletwa miaka 10 iliyopita akiwa na wenzie 10, inadaiwa aina yake wamebaki wawili tu. Aina hii ya kifaru kutoka nchini Czech Republic ni faru weupe.

Kwa mujibu wa mtandao wa Natgeo, lengo la kuwaleta faru hao ni kuwapa mazingira stahili ambayo ni pamoja na hali ya hewa, uwanda mpana ili wapate nafasi ya kuishi muda mrefu na kuzaliana kwa lengo la kuokoa kizazi hicho kutoweka kabisa ulimenguni.

Hata hivyo lengo hilo halikufanikiwa na sasa faru hao wamebakia wawili tu ulimwenguni. Miaka michache iliyopita kundi la wanasayansi likishirikiana na taasisi mbalimbali za utafiti pamoja na Taasisi ya Huduma ya Wanyamapori Kenya, wamefanikiwa kutengeneza chembe hai za uzazi kwa kutoa katika mayai ya vifaru wa aina hiyo watatu waliokufa pamoja na vinasaba kutoka katika madume yaliyokufa.

Lengo ni kuhamisha chembe hizo zilizohifadhiwa kisayansi kwa faru kama hao ambao hupatikana nchi za kusini ili kupandikiza mimba za faru hao weupe siku za baadae.