May 20, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

KUTAMBUA WAHALIFU WANAOTUMIA MITANDAO YAKO YA KIJAMII BILA RIDHAA YAKO

Mwandishi: Ismail Mayumba

Mitandao ya kijamii ni majukwaa ya mtandaoni yanayowezesha watu kuwasiliana, kushirikiana taarifa, na kuunda au kusambaza maudhui kama maandishi, picha, video, na sauti. Mitandao hii imekuwa sehemu muhimu ya maisha ya kila siku ya watu wengi duniani, kutokana na uwezo wake wa kuwaunganisha watu kwa haraka na kwa urahisi, bila kujali mahali walipo

Kutokana na umuhimu huu, wahalifu wa mtandaoni (wadukuzi) wamekuwa wakitumia akaunti za watu wengine bila ridhaa yao. Madhumuni yao ni pamoja na:
– Kupeleleza taarifa binafsi,
– Kuiba utambulisho wa mtu kwa ajili ya kufanya uhalifu,
– Kuchukua kabisa umiliki wa akaunti na kudai fidia ili kuirudisha,
– Au hata kuitumia akaunti hiyo kumchafua mhusika.

Kwa bahati nzuri, mitandao ya kijamii imeweka njia za kukusaidia kutambua na kuondoa vifaa visivyo halali vinavyotumia akaunti yako. Ingawa mbinu zinatofautiana kwa kila mtandao, hapa chini tumeangazia mitandao mikubwa na jinsi ya kujilinda:

WhatsApp

  • – Fungua WhatsApp.
  • – Gonga alama ya vidoti vitatu (kushoto juu) kisha chagua Linked Devices.
  • – Utaona orodha ya vifaa vilivyounganishwa na akaunti yako.
  • – Kama kuna kifaa usichokitambua, bonyeza Log out ili kukiondoa.

Facebook

  • – Fungua app ya Facebook.
  • – Nenda kwenye Menu > Settings & Privacy > Settings.
  • – Chagua Password and Security, kisha Where You’re Logged In.
  • – Hapa utaona vifaa vyote vinavyotumia akaunti yako.
  • – Bonyeza alama ya nukta tatu upande wa kifaa usichokitambua, kisha Log Out.

Instagram

  • – Ingia kwenye akaunti yako ya Instagram.
  • – Gonga kwenye Menu, kisha nenda Accounts Centre.
  • – Fuata hatua sawa na Facebook kuangalia na kuondoa vifaa visivyo halali.

Telegram

  • – Fungua app ya Telegram.
  • – Gonga alama ya menyu (mistari mitatu juu kushoto).
  • – Nenda Settings > Devices.
  • – Utaona vifaa vilivyounganishwa – bofya kifaa usichokitambua na ondoa ili kuhakikisha usalama.

TikTok

  • – Fungua TikTok na nenda kwenye Profile yako.
  • – Gonga menyu (alama ya mistari mitatu) > Settings and Privacy.
  • – Nenda Security and Login > Manage Devices.
  • – Tazama orodha ya vifaa – toa vifaa visivyo vya kwako

Mitandao ya kijamii imeweka njia hizi mahsusi ili kukulinda dhidi ya matumizi mabaya ya akaunti zako. Ni muhimu kufuatilia mara kwa mara vifaa vilivyounganishwa ili kuhakikisha usalama wa taarifa zako binafsi. Usisite kuchukua hatua haraka pindi unapogundua kifaa au shughuli isiyo ya kawaida.