January 22, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kusaga afunguka Clouds FM kupiga nyimbo za Lady Jaydee

Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online

BOSI wa redio Clouds Jaseph Kusaga amesema, yeye hana ugomvi na msanii mkongwe katika muziki wa Bongo fleva kwa upande wa wanawake Judith Wambura maarufu ‘Lady Jaydee’ hivyo haoni sababu ya kuacha kupiga nyimbo zake.

Akizungumzia hilo leo kwenye kipindi Cha XXL Ya Clouds fm Kusaga amesema, mbali na na nyimbo za Lady Jaydee kupigwa katika Redio hiyo bali ameitaka pia kupiga nyimbo za wanamuziki wengine.

”Mimi sijawahi kuwa na matatizo na Lady Jaydee, hata sijui chochote na kuhusu kucheza nyimbo zake kwanini msipige na za wengine, kwanini msiwe sawa na wengine,” amesema Kusaga.