January 23, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kukamilika ujenzi daraja la Mpanda kutakuza uchumi

Na George Mwigulu,Timesmajiraonline, Mpanda.

KAIMU Meneja wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mjini (TARURA) Mkoa wa Katavi Mhadisi Paschal Sindani amesema kukamilika kwa ujenzi wa daraja Kawaliyowa Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi utaunganisaha jamii na kukuza uchumi.

Mha.Sandani amesema hayo akitoa taarifa ya ujenzi wa daraja hilo leo Septemba 12, 2024 kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2024, Godfrey Mnvazau ambapo amesema daraja hilo litawezesha upatikanaji wa huduma muhimu kama vile afya, elimu na masoko hasa kwa jamii zilizo mbali na huduma hizo.

Amesema kuwa licha ya daraja hilo kuwa msaada zaidi kwa wanafunzi ambao walishindwa kufika shuleni hususani wakati wa mvua kunyesha wakati wa masika pia utakuwa ni kichocheo cha usalama kupitia ulinzi na raia kwa kurahisisha upatikanaji wa huduma za usalama na misaada ya kibinadamu.

“Ni muhimu kufahamu kuwa uwepo wa daraja hili unatoa fursa ya ajira kwa vijana kupitia shughuli za bodaboda na huko ndio maana ya kukuza uchumi” Amesema.

Mha.Sindani, ameeleza kuwa gharama ya mradi wa ujenzi wa daraja hilo hadi kukamilika ni fedha zaidi ya Mil 475 zimetumika.

Mbunge wa Jimbo la Mpanda Mjini, Sebastian Kapufi amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha zilizotumika kujenga daraja ambalo ni muhimu kwa maendeleo ya watu.

Kapufi ameeleza kuwa kukamilika kwa daraja hilo unafungua fursa kwa wananchi kufanya kazi za kujenga uchumi pasipo na tatizo lolote huku akiwaomba wananchi kutunza miundombinu ya daraja hilo.

Kwa upande wa Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2024, Godfrey Mnzava amelishwa na ujenzi wa mradi huo wa daraja na kuwaomba wananchi kuulinda.