Na Penina Malundo,TimesMajira,Online
KAMISHNA mstaafu wa Jeshi la Polisi nchini, Suleiman Kova amesema licha ya kuwa amestaafu, lakini bado anauhitaji wa kuendelea kuwatumikia Watanzania.
Akizungumzia leo jijini Dar es Salaam katika Mkutano wa Mtandao wa Nguvu ya Pamoja ya Wanawake ( Women Tapo) Kova amesema, licha ya kustaafu, lakini bado anaendelea kufanya kazi na watanzania katika nyanja mbalimbali.
“Nimestaafu bado nawapenda watanzania wenzangu, bado nataka niwatumikie na ndio maana nimeanzishaa taasisi yangu ambayo inanifanya niwe karibu na watanzania wenzangu,”amesema.
Mwenyekiti wa Women Tapo,Stella Mbaga amesema kutokana na wanawake kuwa na mchango mkubwa katika jamii wameamua kuwaletea vifaa vya kunawa mikono katika kupambana na maambukizi ya ugonjwa wa corona.
“Msaada huu tumepata kutoka katika Mfuko wa Wanawake, hivyo tukasema tuwaletee ili nanyi muendelee kujikinga na corona hapa sokoni (Soko la Tabata),”amesema.
More Stories
Uongozi wa Rais Samia wapeleka neema MNH
Johari:Tunataka kuwa champion wa dira ya taifa ya maendeleo ya 2050
TRC yakamilisha majaribio ya mabehewa ya mizigo ya SGR