Na Zainabu Jambia, Timesmajira Online MTWARA
MKURUGENZI Mkuu wa bodi ya korosho Tanzania Francis Alfred amesema kuwa mpaka kufika sasa wameshakamilisha taratibu zote kuelekea korosho Marathon.
Ameyasema hayo leo august 28 alipokuwa na waandishi wa habari mkoani mtwara ambapo amewataka wananchi na wadau wote wasiojisajili wajisajili ili kuweza kushiriki kwa pamoja katika mbio hizo.
“Tuko tayari kwaajili ya kwenda kwenye korosho marathon kwahivyo tunawaomba wananchi pamoja na wadau wote kushiriki” amesema mkurugenzi huyo
Aidha amesema kuwa pamoja na mbio hizo kutakuwa na burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali , mgao wa korosho , pamoja na kutoa zawadi kwa washindi.
Hata hivyo ameongeza kuwa gharama ni shilingi elf 30 ambayo itatumika katika usajili huo ili kuweza kupata vifaa vya mbio ikiwa nj pamoja na tishrt.
“Niwaombe wananchi na wadau wote tukamikishe taratibu za usajili ikiwa ni pamoja na kulipia shilingi elf 30 itakayo tumika katika vifaa vya mbio hizo” alisema mkurugenzi francis
More Stories
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba