January 6, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un akishuhudia majaribio ya makombora nchini humo Machi 21, 2020

Korea Kaskazini yasifu jaribio lake

PYONYANG, Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Korea imesifu jaribio lake la makombora ililolifanya juzi, ikisema lilikuwa la aina yake.

Shirika la habari la Serikali, KCNA, lilieleza jana kuwa,mfumo huo uliojaribiwa umefanikiwa na kwamba sasa utakabidhiwa rasmi kwa jeshi la nchi hiyo.

Kwa mujibu wa shirika hilo la habari, lengo la jaribio hilo lilikuwa ni kuangalia masuala ya kiteknolojia na kiufundi ya mfumo huo.

Juzi Korea Kaskazini ilirusha makombora mawili ya masafa mafupi kuelekea Bahari ya Japan, kwa mujibu wa jeshi la Korea Kusini, ambalo pia limesema makombora mawili yaliyorushwa kutoka pwani ya mji wa Mashariki wa Wonsan yaliruka kwa masafa ya kilomita 230.

Aidha, hiyo ilikuwa ni mara ya nne kwa mwezi huu kufanywa majaribio hayo yaliyokuwa yamesitishwa kwa miezi mitatu.