April 1, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kongamano ‘eLearning Africa’ kufanyika Mei 7,2025 Dar

Na Zena Mohamed,Timesmajiraonline,Dodoma

WAZIRI wa Elimu Sayansi na Teknolojia Perof.Adolf Mkenda amasema Tanzania nchi mwenyeji wa kongamano la kimataifa la eLearning Africa linalotarajiwa kufanyika Mei 7 hadi 9,2025 katika kituo cha mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es salaam.

Mkenda amesema hayo jijini hapa leo,Machi 29,2025 wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ujio wa kongamano hilo ambapo amesema litakuwa la mara ya pili kufanyika nchini.

Ametaja lengo la kongamano hilo kuwa ni kuleta kwa pamoja makundi mbalimbali kutoka zaidi ya nchi 65 kwaajili ya kujadili,kubadilishana uzoefu,kuhamasisha uwekezaji na kuazimia mipango ya pamoja ya kuchagiza matumizi ya Teknolojia za kidijitali katika sekta ya Elimu barani Afrika.

“kongamaono la 18 la eLearning Africa litafanyika katika kituo cha kimataifa cha Julius Nyerere jijini dar es salaam kuanzia mei 07 hadi 09 mwaka huu,tangu kuasisiwa kwake mwaka 2005 kongamano hili lishafanyika nchi 17 ikiwemo Tanzania.

“Tanzania lilifanyika mwaka 2021 hivyo mwaka huu litakuwa linafanyika kwa mara ya pili,kongamano hili linalenga kuwakutanisha wadau kutoka zaidi ya 65 barani Afrika”,amesema.

Aidha amesema makundi hayo ya wadau yatajumuisha watunga sera,watoa maamuzi,wataalamu wa Elimu,wataalamu wa Teknolojia,watafiti,wabunifu,wafanya biashara,wawekezaji na wadau wa maendeleo.

Aidha amesema kongamano hilo litajumuisha mkutano wa mawaziri zaidi ya 50 kutoka nchi 49 barani Afrika utakao kuwa na lengo la kuazimia mikakati ya pamoja na kuandaa nguvu kazi maili katika kubuni, kuzalisha,na kuimalisha matumizi ya kidigitali.

“Kama wenyeji wa kongamano hili nchi yetu inatarajia kunufaika na fursa mbalimbali  kutokana na kuwa mwenyeji wa kongamano hili ambapo tutabaini mikakati mpya hususani katika sekta ya Elimu”,amesema.

Kongamano hilo litaenda sambamba na kaulimbiu isemayo “kufikilia upya Elimu,na maendeleo ya raslimali watu kwa ustawi wa Afrika”