January 9, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Klabu za waandishi zatakiwa kupigania haki za waandishi

Na Judith Ferdinand,TimesMajira Online,Mwanza

KLABU za waandishi wa habari nchini,zimeombwa kuwa mstari wa mbele kupigania maslahi na haki za waandishi wa habari.

Hayo yamezungumzwa na Mratibu wa Programu wa shirika la kihabari la Internews Shabani Maganga,wakati alizungumza kwenye mkutano wa kimtandao wa kutathimini mwenendo wa vyombo vya habari kwa robo ya pili ya mwaka 2021.

Ambao mkutano huo umeandaliwa na Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mwanza(MPC),ikishirikiana na taasisi ya Kihabari ya Internews.

Maganga amesema,kila mwandishi wa habari kwa nafasi yake afanye kazi lakini pia klabu za waandishi wa habari kama taasisi ambazo zinawasaidia waandishi wa habari wawe mstari wa mbele kupigania maslahi na haki za kundi hilo.

Amesema,changamoto zote zilizozungumzwa klabu za waandishi wa habari wawe mstari wa mbele kuzitatua,na wao kama Internews na taasisi mbalimbali zipo tayari kushirikiana nao kufanya kazi pamoja .

Pia amesema,waandishi wa habari ni kundi muhimu na wadau wakubwa katika jamii basi watumie nafasi hiyo kutatua changamoto zinazo wakabili.

Mratibu wa Programu wa shirika la kihabari la Internews Shabani Maganga,wakati alizungumza kwenye mkutano wa kimtandao wa kutathimini mwenendo wa vyombo vya habari kwa robo ya pili ya mwaka 2021.

Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi Wizara ya Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Rodney Thadeus,amesema nia ya serikali ni kujikita katika kuvifungulia vyombo vya habari vilivyofungiwa.

Amewataka waandishi kufanya kazi kwa weledi ili kuepuka vyombo vyao vya habari kufungiwa.

Pia amesema,serikali imepokea changamoto zote za wanahabari nchini na itahakikisha inaweka mikakati ya kuzitatua huku waandishi wa habari wawe huru kwenye kusema vikwazo vinavyokwamisha utendaji wa shughuli zao.