Na Esther Macha, Timesmajira Online, Mbarali
BARAZA la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya limemchagua Jeremiah Kisangai kuwa Makamu Mwenyekiti wa halmashauri hiyo ambaye ataongoza kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Akitangaza matokeo hayo leo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali, Raphael Shitindi amesema kuwa kwa mujibu sheria Makamu Mwenyekiti huchaguliwa kila baada ya mwaka mmoja.
Amesema kuwa jumla ya kura 21 zimepingwa kati ya hizo kura za ndiyo ni 19 iliyoharibika ni moja na hapana moja kwa maana hiyo Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali ni Jeremiah Kisangai ambaye ataongoza halmashauri hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti huyo wa Halmashauri hiyo aliyechaguliwa,Diwani wa Kata ya Miyomboni , Jeremiah Kisangai amesema l kwa nafasi aliyopewa na kuaminiwa ameomba waendelee kumshauri na kumtumia kwa maslahi mapana ya halmashauri na kuwa sehemu nzuri ya kumshauri Mwenyekiti wao Twalibu Lubandamo.
“Nitaendelea kujenga mshikamano na umoja baina yetu Madiwani, ofisi ya Mkuu wa Wilaya pamoja na viongozi wote ngazi ya halmashauri, mimi ni binadamu kwa nafasi ambayo mmeniamini naombeni mnitumie katika kunishauri kwa maslahi mapana ya halmashauri yetu,sasa kama kuna jambo la kushauri ni vizuri kuelezana,”amesema Makamu Mwenyekiti Kisangai.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Rujewa Jeremiah Makao amesema kuwa uchaguzi uliofanyika wa kumpata Makamu Mwenyekiti mpya unaenda kuwa chachu kwa Madiwani katika kushirikiana kwa pamoja katika usimamizi wa kazi za halmashauri.
More Stories
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba