Na Penina Malundo,TimesMajira,Online
KATIBU Mkuu Mstaafu wa Chama cha Mapinduzi CCM,Abdulrahman Kinana na Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa waungana na viongozi wengine wa Chama hicho kumuombea kura Mgombea Urais wa Chama hicho,John Magufuli.
Akikaribishwa leo katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid mkoani Arusha na Mgombea Urais wa Chama hicho,Magufuli kuwasalimia wananchi na wanachama waliofika katika mkutano wa Kampeni wa Mgombea Urais huyo,Katibu Mkuu huyo Mstaafu,Kinana amesema kipindi cha miaka mitano iliyopita, Magufuli amefanya mambo makubwa manne ikiwemo kutekeleza ilani kama alivyoahidi mwaka 2015.
Amesema ametekeleza ahadi zake alizozitoa kipindi cha kampeni zake,ametekeleza ahadi alizokuwa anatoa akifanya ziara mikoani na kuwa na ahadi mpya zenye zaidi ya kurasa 303 za kuwahudumia watanzania.
“Nawaomba watanzania wote Oktoba 28 mwaka huu,tumpe kura za kishindo Mgombea wetu wa Urais,,”amesema
Nae Waziri Mstaafu,Lowassa amesema nchi ya Venezuela na Nigeria zinafujo kwa sababu ya mambo ambayo yanaleta amani katika nchi yetu.
“Kupitia kwa Mwenyezi Mungu,Rais wetu amepewa jukumu la kuangalia mambo katika nchi hii amekuja na ndoto sahihi kwamba madhara hayo hayaji kwetu…amejitahidi na wananchi wameelewa,”amesema
Lowassa amesema sasa wananchi wampe zawadi Rais Magufuli na zawadi yenyewe iwe kura ifikapo Oktoba 28,2020.
*** Viongozi wa dini wanena
Akizungumza katika Mkutano huo,Sheikh wa Mkoa wa Arusha,Sheikh Shabani Jumaa
amesema amani ndio kinga ya kweli katika kuulinda mwanadamu na ubinadamu.
Amesema Mwanadamu ndio mtakatifu kuliko vitakatifu vilivyowahi kuumbwa na Mungu,kutoka na umuhimu wa amani inatupaswa kujifunza kutoka kwa mitume wa Mungu.
“Mazungumzo kuhusu amani ni makubwa na mengi hivyo tunapaswa kujifunza amani kutoka kwa Mwenyezi Mungu na tunapaswa kuomba amani ambayo inatoka kwa Mungu,hivyo amani aliyopo tuiendeleze kabla na baada ya uchaguzi Mkuu unakuja,”alisema
Naye Askofu wa Kanisa la Katoliki Dayosisi ya Arusha,Isack Amani amesema Mungu abariki uchaguzi Mkuu uliombele kwa njia ya kura na kupata viongozi atakaowaweka Mungu.
“Tunaomba Mungu utupatie viongozi watakaosimamia tunu,misingi ya taifa ambazo ni umoja ,upendo,haki kwa wote na ustawi kwa kila mtu,”amesema Askofu Amani
Pia amesema Mungu asaidie uchaguzi Mkuu ufanyike kwa uhuru,usalama ,uwazi na baada ya uchaguzi watu washirikiane na viongozi watakaochaguliwa kukaa kwa amani na mshikamano wa kitaifa.
More Stories
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba