January 10, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kinana :CCM inaunga mkono juhudi na malengo ya Serikali

Na Penina Malundo,timesmajira,Online
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana, amesema Chama kinaunga mkono juhudi na malengo ya serikali katika kuenzi, kutunza na kuendeleza historia ya ukombozi wa Afrika.
Kinana ameyasema hayo leo, alipotembelea ofisi za Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika, na kujionea hatua mbalimbali zilizofikiwa katika kuboresha majengo yake na kutunza kumbukumbu muhimu.

Aidha, amewaomba Watanzania kutembelea kituo cha historia ya ukombozi kilichopo Dar es Salaam kwa ajili ya kujifunza na kujua kazi kubwa iliyofanywa na wapigania uhuru na wana ukombozi wa Afrika, huku Tanzania kikiwa kitovu cha harakati hizo.
“Ukombozi wa Afrika walioshiriki ni wengi, nchini zilitoa michango kwa namna mbalimbali, lakini shughuli zote hizi ziliongozwa na mtu mmoja bingwa wa mikakati anaitwa Mwalimu Julius Nyerere,”amesema na kuongeza
Ziara hiyo aliambatana na Waziri wa Michezo, Sanaa na Utamaduni, Mohammed Mchengerwa pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Said Yakubu.