March 8, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kimwanga, achukua na kurudisha fomu Udiwani Makurumla

Akabidhi fomu kwa Katibu wa Kata wa CCM Makurumla, Omari Suleiman Bakari

Akizungumza baada ya kukabidhi fomu hiyo, Kimwanga ambaye pia ni mwanahabari alisema kuwa anajivunia kazi kubwa aliyoifanya kwa miaka mitano na sasa anaomba fursa kwenye kukamilisha maeneo yaliyobaki ili kujenga jamii yenye ustawi.

“Ninamaliza miaka mitano ya mafanikio ambapo sisi Makurumla tumefanikiwa kutekeleza miradi ya zaidi ya bilioni 18 ikiwamo barabara, kituo cha afya na elimu.

“Miaka mitano ijayo tunakwenda kujenga kata yenye kasi zaidi na muonekano mkubwa wa maendeleo kwa jamii, wana Makurumla na wana CCM ni watu wema sana nyakati zote tumekuwa pamoja na Mungu akipenda ikiwa chama itawapendeza jina likarudi kwenye uteuzi sina shaka na maamuzi yao kwangu na chama chetu ni ushindi,” amesema Kimwanga