December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kimara Sekondari yawa kinara zawadi za shule zilizofanya vizuri Ubungo

Na Mwandishi Wetu,Timesmajira Online

SHULE ya Sekondari Kimara, imeibuka kinara baada ya kupata zawadi kwa shule zilizofanya vizuri Manispaa ya Ubungo, jijini Dar es Salaam.

Hafla ya utoaji wa tuzo hizo zimefanyika leo, katika ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.

Afisa Elimu wa Manispaa hiyo, elimu ya Sekondari Vista Mgina ambaye alimwakilisha
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa, ametoa tuzo kwa shule zilizofanya Vizuri katika matokeo ya Kidato cha Pili na cha Nne kwa mwaka 2023.

Katika tuzo hizo, Kimara Sekondari imepata tuzo mbili ambapo mshindi wa kwanza Kidato cha pili na mshindi wa Pili kidato cha nne.